MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

NDEGE ILIYOBEBA WATU 81, WAKIWEMO WACHEZAJI WA KLABU MOJA YA SOKA NCHINI BRAZIL YAANGUKA


Ndege iliyobeba watu 81, wakiwemo wachezaji wa klabu moja ya soka ya Brazil, imeanguka eneo la Medellin nchini Colombia.

Maafisa wa usalama wanasema watu sita wamenusurika na ndege hiyo inayodaiwa kupata hitilafu za mfumo wake wa umeme.

Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Bolivia na ilikuwa imewabeba wachezaji wa timu ya Chapecoense, ambao walikuwa wamepangiwa kucheza mechi ya fainali ya Copa Sudamericana, dhidi ya timu ya Medellin, Atletico Nacional.

Taarifa zinasema ndege hiyo muundo wa British Aerospace 146 ambayo imekuwa ikitumiwa na shirika la ndege la Lamia la Bolivia ilikuwa na abiria 72 na wahudumu tisa na ilianguka eneo la milimani nje kidogo mwa mji wa Medellin majira ya saa sita usiku saa za huko (saa mbili asubuhi Afrika Mashariki).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa uwanja wa ndege, marubani walisema ndege hiyo ilikuwa imepata matatizo katika mfumo wake wa umeme.

Maafisa wa uwanja wa ndege wa Jose Maria Cordova de Rionegro uliopo Medellin, wamesema juhudi zote zinafanywa kuwaokoa manusura ingawa hali mbaya ya hewa inazuia maafisa kufikia eneo la mkasa kwa urahisi.

Hakukutokea moto baada ya ndege hiyo kuanguka, jambo ambalo linaibua matumaini ya kupatikana kwa manusura na Maafisa wa uokoaji wanaweza tu kufika eneo la ajali kwa barabara

Meya wa Medellin Mayor Federico Gutierrez amesema ajali hiyo ni "janga kubwa".