RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SERIKALI YATOA MCHANGANUO FEDHA ZA MAAFA KAGERA, HADI SASA AHADI NA FEDHA TASLIMU NI BILIONI 12.1



SERIKALI kupitia ofisi ya Waziri Mkuu leo imetoa mchanganuo kuhusu maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea maeneo ya kanda ya ziwa hasa Mkoa wa Kagera mnamo Septemba 10, 2016.

Mchanganuo huu umetolewa baada ya kuwepo minong’ono mingi hasa kupitia mitandao ya kijamii juu ya kiasi halisi kilichopatikana kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa tukio hilo.

Katika taarifa iliyotolewa leo ni kwamba fedha taslimu kiasi cha shilingi bilioni 5.4 tayari kimeishapokelewa kupitia benki, shilingi milioni 17.6 zimepokelewa kupitia mitandao ya simu huku ahadi zikiwa ni shilingi bilioni 6.7 na kufanya jumla ya ahadi na fedha taslimu hadi sasa kuwa bilioni 12.1.

Kufuatia tathmini za wataalamu, makadirio ya awali yaliainisha kuwa takribani kiasi cha shilingi bilioni 104.9 zinahitajika katika kukabiliana na kurejesha hali katika Mkoa wa Kagera kufuatia maafa hayo.