RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

VIDEO: ‘KATIKA WATU AMBAO HAMTAINGIA MBINGUNI NI WATU WA ARDHI’- RC MAKONDA



November 22 2016 ziara ya Mkuu wa mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda iliendelea kwenye viwanja vya Zakhem Mbagala, lengo ikiwa ni kutafuta majibu ya kero za wananchi, hapa alikutana na kero ya mwananchi ambaye alivunjiwa nyumba yake toka mwaka 1988 na mwakilishi wa idara ya ardhi kutoka manispaa ya Temeke alipopewa nafasi ya kujibu hakutoa majibu yaliyomridhhisha RC Makonda.

‘Ninyi watu wa ardhi ndio maana mnaona viongozi kama vichaa vile, hivi ujanja mtaacha lini? mzee kama huyo tangu mmvunjie 1988 miaka yote hiyo mpaka leo mzee wa watu bado ana maumivu kwenye moyo wake, mnasema mzee leta vithibitisho, mnamtengeneza mahali ambapo hawezi kuwa na nyaraka mnazozitaka ninyi ili ashindwe, mnajua katika watu ambao hamtaingia mbinguni ni watu wa ardhi’- RC Makonda 

Unaweza kuangalia video hii hapa chini



VIDEO: Vituo vya polisi 20 vitakavyojengwa DSM, kimoja kitajengwa hapa


VIDEO: ‘Wenye akili ndogo ndio walilalamika’ – Paul Makonda