WAENDESHA BAJAJI WENYE ULEMAVU WAFUNGA BARABARA DAR


Dar es Salaam: Waendesha Bajaji wenye ulemavu wanaofanya shughuli zao katika Jiji la Dar es Salaam wamelazimika kufunga barabara ya Mission na kuzuia magari kuingia katika ofisi za Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.

Wamefanya hivyo kwa lengo la kushinikiza wapewe vituo maalum vya kupakia na kushusha Abiria katikati ya jiji.