MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

07.12.2016: MC. JOSHUA MAKONDEKO AWASHA MOTO USIOZIMIKA KATIKA SHILOH TANZANIA 2016 NDANI YA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Tanzania MC. Joshua Makondeko mzee wa TutapitaKatikatiYao - No Limit siku ya Jumatano 07.12.2016 aliwasha moto usiozimika katika kusanyiko la kihistoria la SHILOH TANZANIA 2016 linaloendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" mpaka siku ya Jumapili 11.12.2016. Nakuambia palikuwa hapakaliki kabisa ndani ya nyumba ya Mungu. Uimbaji wake ulitawaliwa na nguvu za Mungu ambazo ziligusa kila nafsi ya mtu. Watoto wa Mungu walionekana na furaha na kicheko kwa uimbaji wa mtumishi huyu.


Kumbuka SHILOH hii hufanyika mara moja tu kwa mwaka mzima, na mwaka huu itahitimishwa 11.12.2016, kwahiyo unaombwa sana kufika kupokea majibu yako. Katika Shiloh hii kuna sanduku la mahitaji na maombi lilowekwa maalum kwaajili yako kuandika mahitaji yako au maombi yako ambayo utayatumbukiza katika sanduku hilo, yataombewa na baadae kuchomwa moto. baada ya hapo utasuburia majibu kutoka kwa Mungu mwenyewe. Watu wengi sana wamefanya hivyo katika Shiloh zilizopita na wamepokea majibu yao.


Yawezekana wewe unapitia jambo fulani na hujaona mpenyo wa mafanikio, kila ukijitahidi kutumia akili zako kutatua shida yako hufanikiwi, sasa siku ya leo unagana na watu wa Mungu waliojitoa kwaajili yako kukuombea.


Shiloh hii ikawe suluhisho la shida zako kama utaamini na kutiia sheria za Mungu kwa kusoma Neno lake na kulifanyia kazi, kushika amri kumi za Mungu, kujitoa kwa kazi ya Mungu, kufunga na kuomba, kujitakasa na mabaya, kumpenda mwenzako, kuwatii watumishi wa Mungu wanavyokuagiza, kuiheshimu madhabahu ya Mungu, kuepukana na majivuno, kiburi, usengenyaji, chuki, tamaa, usinzi, ulevi, tamaa na mengine mabaya kama hayo, ukiachana nayo utaone neema ya Bwana ikikujilia. Mwaka 2017 utakuwa ni mwaka wako wa kicheko. Mungu akubariki sana.