RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

07.12.2016: MCH. DICKSON WA KANISA LA MLIMA WA MOTO GEZAULOLE AELEZEA FAIDA ZA KUTUMIA MAFUTA YA UPAKO YA SHILOH TANZANIA 2016 KATIKA IBADA YA SHILOH MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Mch. Dickson kutoka kanisa la Mlima wa Moto Gezaulole siku ya Jumatano 07.12.2016 katika ibada ya SHILOH TANZANIA 2016 inayoendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" mpaka siku ya Jumapili 11.12.2016 aliweza kuwatangazia juu ya umuhimu wa kutumia mafuta ya upako ya SHILOH TANZANIA 2016 ambayo yameombewa na mtumishi wa Mungu Bishop Dr. Gertrude Rwakatare pamoja na jopo la wachungaji wa kanisa hilo. Mafuta haya ambayo yamefanyika baraka kwa walio wengi waliojaribu kuyatumia kwa imani wameweze kupokea kile walichokihitaji na wengine wanasubiria wakati wa Mungu ukifika wapokee baraka zao. Mafuta yanapatikana katika kanisa hili la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Mafuta haya yatafanya kazi kwa msaada wa Yesu kama utakuwa na imani juu ya Mungu kuwa anaweza yote kwa kupitia mafuta haya. Tunaona Musa alitumia fimbo, Paulo na Sila walitumia nyimbo na wakapata kile walichokuwa wakikihitaji. Mungu ana njia nyingi sana za kushusha muujiza wake. Mungu amempa maono haya mtumishi wake Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ili kuokoa mioyo ya watu kutoka katika mateso.

Mungu akusaidie sana ujipatie mafuta na uone kama Mungu atakuacha hivihivi. Pia unatakiwa kujitakasa na kutofanya maovu, kumpenda Mungu na watu wote, kuungama dhambi zako na kutozitenda tena, kufanya maombi na kufunga, kuonyesha upendo kwa kila mtu na matendo mengi mema, na ukifanya hivyo utaona Mungu akinyoosha mkono wake uliobeba baraka kwaajili yako na watu wanakuzungukla.

Tunakuomba sana usikose vipindi vya Shiloh vinavyoendelea hapa kanisani: Saa 4 asubuhi hadi 8 mchana ni maombezi na saa 9 mchana hadi 12 jioni ni Ibada Kuu ya Shiloh na wanenaji wakuu ni Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Bishop Dunstan Maboya, Rev. Ndeda na Mch. Noah Lukumay. Pia kuna wachungaji mbalimbali kutoka mikoani watakuombea. Usikose baraka hizi.