RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

09.12.2016: WAZEE WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" WAPIGA PICHA YA KUMBUKUMBU KWAAJILI YA SHILOH SIKU YA IJUMAA

Wazee wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na wachungaji wa kanisa hilo siku ya Ijumaa ya SHILOH TAnzania waliweza kupiga picha ya kumbukumbu kwa utukufu wa Mungu.

SHILOH Tanzania ni kusanyiko la watoto wa Mungu ambalo hufanyika mara moja tu kwa mwaka. Watu hukusanyika pamoja na kumuomba Mungu afungue milango katika maisha yao. Kwa mwaka huu SHILOH imezinduliwa rasmi 04.12.2016 na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akishirikiana na Bishop Dr. Dunstan Maboya kutoka Arusha na kuhudhuriwa na watu kutoka katika mikoa 24 ya Tanzania. 

Rev. Ndeda kutoka Afrika naye aliweza kuhudhuria kusanyiko hili na kufundisha kuondokana na umaskini ambao unatesa sana watu wengi, kwani na yeye ni miongoni mwa watu walioishi maisha ya umaskini sana akiwa nchini Kenya, lakini sana sasa ni miongoni mwa matajiri wakubwa nchini Afrika Kusini.

Shiloh hii itahitimishwa Jumapili 11.12.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usaifiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa, utaona magari ya Mlima wa Moto Mikocheni "B".