RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

25.12.2016: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ATOA UJUMBE MZITO SIKU YA KRISMASI ATAKA UTAMBUE UTAFANYAJE KUENDELEA NA MAISHA YA KUMTUKUZA MUNGU BAADA YA KUZALIWA KWA YESU KRISTO

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Krismasi 25.12.2016 aliweza kutoa ujumbe mzito sana wa kuzaliwa kwake Yesu Kristo, alikuwa na haya ya kusema, “Unajua mamajusi walitoka mbali kuja kumuona mtoto Yesu. Yesu alikuja ili aweze kukaa na wanadamu. Sasa leo Yesu amezaliwa ili akae na wewe.  
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Yesu amezaliwa sasa inatakiwa uendeleeje na huyu Yesu? Unatakiwa kumshika huyu Yesu katika maisha yako. Yesu amezaliwa na ameingia moyoni mwako, na sasa anakaa na wewe. Yesu ni mgeni rasmi katika nyumba yako siku ya leo ya Krismasi. Soma kitabu cha Luka 2:41. Sisi tunajiita Wakristo kwasababu tumempokea kuwa Bwana na Mwokozi wetu. Siku ya leo Kristo anataka kukaa pamoja na wewe.
Furaha Isaya na Rose Rwakatare (kulia)

 Ukimpokea Kristo anasema Yeye Baba anakaa ndani yetu. Lakini watu tunavyosherekea Krismasi tunakuwa ni watu tunayepokea mambo juujuu na sio mambo ya ndani. Sasa kwasababu Krismasi hii ni mwaka mpya Kiroho,basi andika “My New Year of Resolution” andika malengo yako na matakwa yako, andika yale ya mwaka jana yaani 2016 kuwa ulishindwa nini? Mahudhurio yako ya ibada yalikuaje?. Kipindi cha Krismasi ni cha kufanya “Spiritual Inventory”
 
Mwenye duka mara nyingi hukaa kwa wiki mara moja kuangalia ni mali gani inaisha kwa haraka katika duka lake, na katika kwenda kununua vitu vya dukani anaangalia kile kinachouzika sana. Na wewe wakati wa Krismasi ni wakati wa kutengeza upya kiroho chako, ni wakati wa kukarabati maisha yako ya kiroho, ni wakati wa kumwambia Mungu ninaomba unipe nguvu mpya ya kuanza kiroho.
 
Wazazi wa Yesu walikuwa wamemzoea Yesu, kwasababu ni mtoto wako, wakaingia naye kama ilivyo desturi katika eneo la kuabudia na wakaabudu, walipomaliza kuabudu, wakaanza kurudi walikotoka wakijua Yesu ypo katikati ya jamii. 
Wazazi wake wakaenda mwendo wa siku tatu wakiwa wamemsahau mtoto wao (Yesu). Sasa sijui na wewe una miezi mingapi umemsahau Yesu, eti kwasababu umekwazwa. Watu wengi sana wamekwazwa na wakiambiwa twende kanisani wanasema, “Achana nayo, maombi ya nini bwana?” Sasa na wewe unatakiwa kujiuliza umemuacha Yesu kwa ahatua ngapi?
 

Watu wengine wanaamua kuzila kuja kanisani kusali, kumuomba Mungu, kukutana na watakatifu wenzao wanabaki majumbani mwao na wengine wanasema wao wanasali kwenye TV. Na hii ni kutokana na kukwazika na kumesababisha kuumia moyoni mwake.”
 
Watu wengine wanampokea Yesu na wanaishi naye kwenye maombi, kwenye kusifu n.k lakini watu hao hao wana “private live”, na wengine wanadiriki kusema, “Nina maisha yangu ya siri”, nina vitu vinenge sitaki Yesu aviguse. 
Mtu huyo ambaye anasema yeye ana “Private Live” akikabwa anaanza kumtafuta Yesu. Watu wametenga maeneo Fulani ya kuficha viasira vyao, nap engine ni kiasira cha Kikulya au cha Kinyakyusa. Utakuta mtu huyo amepiga magoti kusali lakini ndani yake amesimama, na pengine anakung’ong’a.
 
Ni lazima tuvue utu wa kale na tuvae utu upya. Wakati wa Krismasi ni wa kukaa karibu na Yesu. Na watu wengine wakishabanwa mahali na mambo ya dunia wanaanza kusema Yesu “Im Sorry”. Kama tumeamua kuokoka na kumpenda Mungu basi tumpende Mungu kijumla na mia kwa mia, kusiwe na mahali pa kubakiza katika kupenda Mungu.
 
Watu wengine wakimuona Bishop Dr. Gertrude Rwakatare amependeza wanaanza kuniuliza, “Eti wewe unapendezaga kwaajili ya nani?” na mimi nawajibu, “kwaajili ya Yesu”, wananiuliza tena, “Yesu unamuona?”, nawajibu, “ndio namuona”.
 
Krismasi hii muache Yesu maisha yako, mwambie Yesu ingia ndani ya moyo wangu, ingia kazini kwangu, ingia kwenye nyumba yangu, ingia kwenye ndoa yangu, ingia kwa watoto wangu, Mungu ingia kila mahali na sina mahali ninapoficha mabaya yangu. Ukifanya haya yote na zaidi hapo ndipo Mungu anakuwa pamoja na wewe. Mungu amekuja ili akae na wanadamu na kuwasaidia.
 
Hakuna mtu aliyekaa katika Ukristo na akajuta, lakini anayejuta anakasoro katika Ukristo wake. Nataka nikwambie kuwa kwa Yesu kuna raha, kuna pumziko la kweli, kuna amani ya kweli. Wenzako wanakunywa pombe ili wapate amani lakini wewe unapata amani bure kabisa. 
Amni ya Yeu ni “Permanent”, amani ya Yesu haina majuto lakini amani ya pombe lazima utapigana na mtu, utamaliza pesa na asubuhi unaanza kuhangaika chakula cha kulisha watoto. Amani ya kutafuta ndani ya chupa sio amani ya kweli, ni amani yenye majuto. Nakuomba uje kwa Yesu kwani yeye atakupa amani ya kudumu na ya kweli, utakuwa na furaha hata kama unauzuni.
 
Yesu anasema usinione haya mbele za watu, na mimi nitakuone haya mbele za Baba yangu. Watu wanaona haya kusema, “Mimi Nimeokoka”. Mwingine anaposimamishwa mbele ya watu wakubwa na wenye fedha zao, anaogopa kusema, “Mimi ninasali kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare”.
 

Ni lazima utangaze msimamo wako wa kiimani ili watu wajue. Unatakiwa kuinua bendera ya Yesu ili watu wote wajue kuna walokole katika ile nyumba. Mungu akubariki sana.






























 
















 

 

 






















 Miriam Jackson akisoma neno







 Mch. Elizabeth Lucas