MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

25.12.2016: JOSHUA MLERWA AKONGA WAUMINI WA KANISA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI “B” SIKU YA JUMAPILI YA KRISMASI 25.12.2016. AACHA UJUMBE MZITO KUPITIA WIMBO WAKE

Siku ya Jumapili ya Krismasi, mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Joshua Mlelwa aliweza kuimba katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Katika wimbo wake wa ASANTE alikuwa na haya maneno, ambayo yakubariki, na ukitaka kusikia wimbo wake ingia Yotube na andika Joshua Mlelwa-Asante. Maneno hayo ni kama ifuatavyo:- Hakika wewe ni Baba utendae maajabu, umejawa na huruma, umejawa na rehema. Mimi ninataka niende na wewe kwani wewe ni Bwana wangu. Maisha yangu yawe salama, nifanikiwe maisha yangu, kama Musa uwepo wako uende nami, nikupendeze ewe Jehovah.


Ndiwe uliyenitendea mambo makubwa maishani, nikutafakari wewe Mungu kwa kweli mimi ninashangaa, ninaona raha. Asante Yesu kwa wema wako, asante Baba wewe mkarimu, sina tena mtu mwingine ila wewe Bwana wangu. Moyo wangu wa kusifu Mungu, Roho yangu yakufurahi Mungu wangu.

Sitaacha kuimba, kusifu nmaana sifa za bwana zimo kinywani mwangu. Ulaya nitasema, Marekani nitasifu, mashariki ya mbali nitapaza sauti. 
Haleluya wewe ni Mungu na ubarikiwe, sifa zako zivume.


Mfalme Daudi alisema, leo ni siku ya pekee ni siku ya ajabu. Sanduku la Bwana l;imekuta “Town”, uwepo wa Bwana umekuja “Town”. Leta ngoma, vinanda, magita, filimbi ili sifa za Bwana zivume milele. Naomba mtu mmoja aseme amen, aseme Yesu, naomba mtu mmoja apige makofi.

ASANTE YESU