RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

25.12.2016: KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI YA KRISMASI LILIMUOMBEA MZEE WA KANISA MAJOR MALYA KWA JUHUDI ZAKE KANISANI

Wachungaji na waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili ya Krismasi 25.12.2016 kwa utukufu wa Jehova waliweza kumuombea mzee wa kanisa Major Malywa kwa mambo makubwa anayofanya katika kanisa hili pamoja na familia yake. 
Hakika Mungu anaonekana kupitia bidii za Mzee huyu ambaye amejitoa kikamilifu kufanya kazi ya Bwana kwa mali zake na nguvu zake. Kupitia juhudi zake, watu wengi wameokoka kwa njia ya "indrect" kwani kile alichokitoa ndicho kimechangia jambo likafanyika katika huduma ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". 
Kumbuka hata wewe unayetoa shilingi mbili mbele za Bwana, fedha yako hiyo au mchango wako wowote unaotoa ndio unaosukuma jambo likafanyika katika huduma yako unayoitumikia, kwahiyo usidharau kile unachokitoa mbele za Mungu.

Waumini wote wa kanisa hili pia nao hawachoki kumgusa Mungu kwa jinsi wanavyojituma katika kuujenga mwili wa Kristo kwa mali zao, elimu zao na nguvu zao. wamejitoa ili kazi ya Bwana isonge mbele na watu waweze kuokoka na siku ya mwisho waweze kufika mbinguni.

Furaha ya mtu aliokoka ni kuona watu wanaokoka ili siku ya mwisho wakamuone Mungu huko mbinguni. Kwahiyo kuna njia nyingi ambazo unaweza kutumia kuokoa roho za watu. Unaweza kutumia uimbaji, michango, kuhubiri, kufundisha, uandishi wa vitabu, kufariji, kuigiza, kubuni michezo mbalimbali yenye kuleta utukufu kwa Mungu, na vitu mbalimbali waweza kutumia kuwaleta watu kwa Yesu, kwahiyo unatakiwa kujitambua kuwa wewe uko katika nafasi ipi katika kumtumikia Mungu.


Pia kanisa zima liliweza kumuombea Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwaajili ya ulinzi dhidi ya maadui zake. Sasa tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na katikati ya wiki ni saa 9 mchana hadi saa 1 jioni. Mungu akubariki sana.