RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ALIYEKUWA DAKTARI WA MWINYI, PROFESA MTULIA AFARIKI DUNIA


DAR ES SALAAM: Habari zilizotufikia kutoka Hospitali ya Tumaini zinasema kwamba Profesa Idris Ali Mtulia amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa usingizini.

Afisa mmoja wa Hospitali ya Tumaini iliyopo jijini Dar es Salaam alithibitisha kutokea kwa kifo hicho lakini hakueleza kwa undani alipopigiwa simu na mwanahabari wetu.

“Ni kweli amefariki dunia akiwa usingizini,” alisema bila kufafanua na kukata simu huku baadhi ya wagonjwa wakisema kuwa walikuwa na ahadi ya kuonana naye leo katika hospitali hiyo ili awatibu.

Prof. Mtulia alikuwa daktari bingwa wa kwanza wa moyo nchini na wataalamu wenzake wakampachika jina la utani la Mchawi wa Moyo.

Enzi ya uhai wake, aliwahi kuwa daktari wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, mzee Ally Hassan Mwinyi akiwa madarakani.

Prof. Mtulia pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Mbunge wa Jimbo la Rufiji, aliwahi kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kuanzia mwaka 2002 hadi 2007. Ameacha mjane na watoto sita.