MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

08.01.2017: MCH. NOAH LUKUMYA: FAIDA ZA MTU KUWA NA KIBALI CHA MUNGU MBELE ZA WATU“Maandiko yanasema, ”Akawa pomoja na Yusuph na akamfanikisha katika nyumba ile na alipomfanikisha akapata KIBALI” kila kitu kilichokuwa kimelala kikaamka kwa sababu kulikuwa na kibali ndani ya Yusuph. Pospher alikuwa na wafanyakazi lakini kulikuwa hakuna mwenye kibali kama cha Yusuph, kwa sababu Yusuph alikuwa akiongea kitu mambo yanatiki, yanaenda, na ndivyo mambo mengi yanawezekana kwa mtu mwenye kibali, mtu huyo anakuwa na vita vingi kwa sababu siyo mtu yule wa kawaida bali mtu mwenye, kibali ndani yake. Natangaza kwenye ibada hii ukiona vita viko ndani yako, vinakuzunguka sio kwa sababu nyingine kuna kibali cha Bwana juu ya maisha yako. Ukiona maadui wameinuka usianze kupambana nao wewe pambana jua nina Bwana anayekaa na mimi wala si mimi ninayeishi ila kuna kibali cha Mungu ndani yangu. Ukiona hauna vita jiulize swali kuna nini ambacho kimepungua maana kuna kitu ambacho kimepungua wenye vita ni wenye kibali ndio maana Yusuph alipata vita sio kwa sababu nyingineni kwa sababu alikuwa na kibali. Unapo kuwa na kibali kuna watu watakusemea mabaya, usije ukapambana nao, wacha waseme ila wewe shughulika na Jehova, wacha washindane na yakwao wewe shindana na Bwana, simama na Bwana yeye atasimama na wewe. Maandiko yanasema ya kwamba Mungu akawa na Yusuph kila kitu alichokifanya kilibarikiwa. Natangaza mwaka 2017 ukawe ni mwaka wa kibali kwa jina la Yesu kama unaamini sema Ameni. Sema, “Kibali nakihitaji katika maisha yangu”

Katika Biblia tunaona Yusuph alivyopata kibali, alipata kibali si kwa sababu ya elimu yake, au yeye ni mtoto wa Yakobo, au yeye ni mfungwa, ila kwa sababu anamjua Mungu wake. Maandiko yanasema, “Wale wamjuao Mungu wao, watafanya mambo makubwa”. Ukiwa unamjua Mungu wako, kuna vitu unafanya hata wakuu wako watashangaa na kujiuliza umetoa wapi akili hii? Ufahamu huu unautoa wapi? Kwa sababu siyo mimi ninayeishi ila yupo anayekaa ndani yangu na mawazo yangu siyo ya kwangu ila Jehovah ananisaidia. Ninatangaza utembee na kibali. Sema, “Kibali tembea nami, lala nami, amka nami, kula nami, ishi nami, vaana nani.” Mpendwa ukiwa na kibali unaweza ukavaa nguo yoyote ukapendeza, unaweza kuvaa chochote kikakubali, chakula chako watu watakitamani. “Sema, ”Nahitaji kibali, shuka kwangu”. Unajua nasi tuna kibali na ndio maana tumifika 2017 kwani kuna wengi waltamani kufika lakini hawakuweza kuona mwaka huu. Mungu akupe kibali mwaka 2017kila unachofanya kwa watu na mbele za Mungu kikakubalike. Mambo yako yanakwenda kunyoka, hatakama kuna wapinzani lakini watakupisha wakupe Baraka yako, hata kama wapo wanaokuchukia, watakwambia chukua mlango huu, hata kama kuna wabaya, mbele yao watakuandalia meza ya chakula cha kifalme, hata kama hawafurahi juu yako wewe achana nao , wewe una kibali na kinafanya kazi kwako. Kuna watu watasikia kichefuchefu juu yako achana nao, maana kichefuchefu chao ni kwa sababu ya kibali chako. 

Usishindane na mtu mwenye kibali, mwenye kibali usije ukamdumbukiza kwenye tundu la simba ukadhani umemmaliza, ukimuweka kwenye tundu la simba ana kibali cha simba atapita katika simba utajiuliza imekuwaje? Utashangaa kwa sababu ukimchukua mwenye kibali haangukagi anainama. Natangaza mwaka 2017 hautaolewa kwa sababu ya kitu fulani bali utaolewa kwa sababu una kibali. Mtu mwenye kibali atakosana na watu wote lakini hawezi kukosana na Mungu, mwambie jirani ako usikosane na Mungu wako, wacha watu wakuchawie, watu wakuweke kando lakini wewe ungana na Jehovah. Hata wakikusemea vipi lakini wewe usiachane na Mungu wako, Familia yako inaweza ikanyang’anywa lakini hakuna mtu anayeweza kunyang’anya kibali chako, watu watakunyang’anya cheo lakini siyo kibali. Kuna watu wamenyang’anywa gari lakini hawajanyang’anywa kibali, kuna watu biashara inaharibika, kuna watu ndoa inaharibika lakini sio kibali. Pokea kibali cha Bwana kwa jina la Yesu. Mwaka 2017 hautatembea na nguo nzuri, utatembea na kibali kizuri kwa jina la Yesu, hautatembea kwa sababu unajulikana, utatembea kwa sababu una kibali. Hatuna sura nyingine ya kusema bali kumwambia Mungu tuko kwa ajili yako, hatuko kwa ajili ya vitu vingine, hatuko kwa ajili ya urembo, bali tuko kwa ajili ya kazi ya Bwana yeye aliyetuweka hai, ana mawazo ya kila mmoja.

Tuombe kidogo, “Sema, Ee Bwana Yesu, ninakupa heshima, na utukufu, Ee Bwana Yesu umeniumba nikuabudu, sasa ninasahau yote yaliyoniumiza, yaliyonijeruhi, ninasahau yote yaliyonitesa, ninaleta sifa, ninaleta shukrani za moyo wangu mbele zako. Ee Bwana Yesu ninainua mikono yangu nikisema wewe ni Mfalme, wewe ni Bwana wala hakuna mwingine, wewe ni mwamba wangu unastahili kuabudiwa katika jina la Yesu kristo Ameni.”

Wewe sema nasali tu Mlima wa Moto Mikocheni “B” na utaona mambo yako yananyooka. Wakati Naomi amefiwa na Rutu naye amefiwa, akamwambia “Watu wako watakuwa watu wangu, Mungu wako atakuwa Mungu wangu, mahali utalala na mimi nitalala, mahali utazikwa na mimi nitazikwa”. Alikuwa anamwambia nitatembea na wewe maani nimeona kibali unacho. Nasema hata kama kibali kimezuwiwa na mume lakini hicho kibali chako kitainuka mbele ya Wafalme. Pokea kibali chako kwa jina la Yesu, Wakati wa matatizo ndio kibali kinaonekana. Mungu akupe kibali, mwaka huu 2017, uwe na kibali kikubwa kwako, kama unaamini sema “Nakipokea kibali cha Bwana kwa jina la Yesu”. Ukitaka kufanikiwa unatakiwa kujishughulisha na mtu mwenye matatizo na baada ya kutatua matatizo yake kibali chako kitaibuka zaidi, ukiwa na kibali fedha itakufuata yenyewe maana unacho kibali pokea kibali kwa jina la Yesu.

Kuna mahali ambapo kuna upinzani, mwaka huu akakupe kila kitu unachokihitaji, kuna mtu amekalia kiti chako. Sema, “Kuanzia sasa, aliyekalia kiti changu, kila mahali alipo asimame na anikaribishe nikae,aachie kibali changu hapo na ninatangaza kwa jina la Yesu, watoto wako wapate kibali kwa jina la Yesu. Nasema Mungu atawabeba 2017 mkang’ae kwa safari, mkang’ae kwa pesa katika jina la Yesu kristo. Kama Nabii wa Bwana wa Mlima wa Moto natabili nafasi za kuinuliwa, Bwana akakupe nafasi, akakuinue na kukupa hitaji la moyo wenu. Meshaki, Shadrak na Abednego hawakuwa na “fire tools” walikuwa tu na kibali walipotumbukia tu mle ndani walianza kuongelea na moto unawambia “Hivi mnajua ninyi ni watu wangu wazuri, mnajua ninyi mmechoma wachawi kwa hiyo mimi huwa nashilikiana nanyi?” Unapoamka tu asubuhi usiamke tu kwa kukurupuka, ita kibali kwani kibali huwa kinasikia. Kuna wengine wataitwa ni wachawi, achana nao watasema wewe ni mchawi, lakini kwa sababu wewe unajua unasema siyo uchawi unasema ni Mungu amekusaidia unaposema Mungu amenisaidia unatoka mbele yao unasema mnawaza msiyo yajua maana mimi siyo wa kawaida ninakibali cha Bwana aliyejuu yangu,. Nataka kukwambia ulipo hapo siyo wewe, wanashindana na kibali na kibali chako lakini yatawashida.

Mch. Noah Lukumay