RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

31.12.2016: FAMILIA YA KASEMBE YATOA ZAWADI YA MWAKA MPYA KWA BISHOP DR. GERRTRUDE RWAKATARE KATIKA MKESHA WA CROSSOVER MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Familia ya Bwana Kasembe siku ya mkesha wa kukaribisha mwaka 2017 (CrossOver) katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliweza kutoa zawadi kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kutokana na mchango wake mkubwa katika familia yao na malezi bora ya Kiroho. Akiongea kwa uchungu, Mrs. Kasembe alimshukuru san Bishop kwani amekuwa akijitoa katika kuhudumia kanisa, hakosi kufika ibadani kila Jumapili na katikati ya wiki, amekuwa mstari wa mbele wa kubeba matatizo ya watu, anajituma kwaajili ya jamii na pengine hata kusahau familia yake, yuko kifua mbele kuchomwa mikuki kwaajili yetu, ni mama ambaye anajituma kufanya kazi ya Mungu hata kama umri wake ni mkubwa, ni mama ambaye sio mbaguzi kuanzia kwa wageni wanaofika kuhubiri katika madhabahu ya Mungu ambaye alikabidhiwa kuisimamia na watu wa kawaida wanaofika kuabudu Mlima wa Moto Mikocheni, ni mama anayejitoa kusaidia wagonjwa katika mahosåpitali mbalimbali na pia kuwatoa wafåungwa magerezani.

Baada ya hapo familia ya Kasembe waliwashukuru waumini kwa kuwa pamoja na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa mwaka mzima.

Sasa tukukaribishe katika ibada ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" Jumapili hii kuanzia saa 30 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa, utaona magari ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" au utasikia watu wakisema, "Kanisani kwa Mama Gertrude Rwakatare" Ingia humo na utafikishwa kanisani bila ya nauli kulipia na utarudishwa kituoni baada ya ibada