RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

31.12.2016: KWAYA ZA MLIMA WA MOTO ZAFANYIKA BARAKA KATIKA MKESHA WA CROSSOVER WA KUKARIBISHA MWAKA MPYA 2017

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa wema wake juu ya wanakwaya hawa wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Kwaya hizi ambazo ni Joybringers na Happy Kwaya zimefanyika nguzo katika kanisa hili la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa mchango wao wa uimbaji na wanavyojituma kwa kazi ya Mungu. Wanakwaya hawa wanafanya kazi ya Mungu kama siafu yaani kwa uishirikiano kuhakiksha watu wanabarikiwa na kile wanachokitoa kutoka kwa Mungu.

Siku ya mkesha wa kukaribisha mwaka mpya 2017 (CrossOver) walifanyika baraka sana mbele za watu na mbele za Mungu kwa jinsi walivyojituma katika uimbaji na kucheza. Watu wengi sana waliofika katika mkesha huu walimtukuza Mungu wakiungana na waimbaji hawa.

Jumapili hii watakuwepo katika ibada ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Ni wakati mzuri kwako kupokea baraka za Mungu kupitia uimbaji. Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha Mabasi Cha Makumbusho dar au Mwenge kwenye mataa utaona magari ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" au utasikia watu wakisema kwa Mama. Mungu akubariki sana.