RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

IJUE SCRUB YA MAZIWA NA ASALI KWA NGOZI YAKO!


Watu wengi sasa hivi wameharibika uso vibaya kutokana na hali ya upepo ambao unasababisha ngozi kuwa mbaya na wengi wamejikuta wakibadilisha badilisha mafuta au cream ya kupaka.

Unaweza kujikuta unabadilisha kila aina ya mafuta lakini bado ngozi yako ikawa mbaya tu na usijue la kufanya.

Leo nimekuletea scrub ya maziwa, asali na limao kwa ajili kukupa matokeo chanya ya ngozi yako.

Mahitaji 

-Maziwa ya unga

-Asali

-Juisi ya limao

-Mafuta ya mzaituni au mrozi

Jinsi ya kuchanganya

Changanya kila kitu kwa usawa, kama ni kijiko kimoja cha asali, juisi ya limao na mafuta ya mzaituni au mrozi vyote viwe sawa. Kama umeamua kutumia nusu kikombe, iwe hivyo kwa vyote.

Baada ya kupata mchanganyiko wote, changanya na maziwa ya unga ukoroge mpaka upate mchanganyiko mmoja. Angalia kama unavutika, kama unavutika kama cream, paka kwenye ngozi yako.

Kaa kwa muda wa dakika 15 kisha fanyia masaji taratibu, baada ya hapo osha kuondoa scrub yote. Maziwa yanaifanya ngozi yako kuteleza na kuwa nyororo, inaondoa madhara ya jua na kukufanya uonekane mrembo zaidi.

Asali inaifanya ngozi yako kung’aa zaidi kwani ina kitu kinachong’arisha, limao linakusaidia ku-breach ngozi na kuifanya kuwa ya asili zaidi.

Mafuta ya mzaituni au mrozi yana uwezo wa kuondoa ngozi iliyokufa na kuleta ile inayong’ara.