RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MADAM FLORA ATANGAZA KUACHANA NA ALBUM


Msanii wa nyimbo za Injili Madam Flora (Zamani: Flora Mbasha) amesema mwaka huu utakuwa ni wa mwisho kwake kutoa albam na kwamba atakuwa anaachia single nyingi ili aweze kuwapatia mashabiki zake nyimbo nyingi mara kwa mara.

Akiongea kupitia eNewz Flora amesema kuwa hiyo ndiyo 'plan' yake kwa miaka ijayo huku akitaka mashabiki wanamuona kuwa amekuwa kimya kwa muda mrefu kutambua kuwa muziki wa Injili upo tofauti na muziki wa bongo fleva ndiyo maana inakuwa rahisi kwa wasanii wa bongo fleva kuachia nyimbo mara kwa mara.
Amesema nyimbo za Injili zinahitaji kuwa na muda wakutosha na kumuomba Mungu ili akupatie mashairi mazuri yenye ujumbe ukisema ukurupuke na kuachia nyimbo kila siku utajikuta unatoa albamu nyingi lakini hit song ni moja na nyimbo nyingine zinasindikiza.