MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MKUU WA WILAYA AJIUZULU MWENYEWE


Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Uyui Bw.Gabriel Mnyele akizungumza na wanahabari na makada wa CCM baada ya kutangaza kujiuzulu wadhifa huo.

TABORA: MKUU wa Mkuu wa Wilaya ya Uyui, iliyoko mkoani Tabora, Gabriel Mnyele ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo kwa hiyari yake mwenyewe baada ya kumwandikia rais Dkt. John Magufuli barua ya kuomba kuachia ngazi kwenye nafasi yake hiyo.

DC Mnyele alipata fursa ya kuwaaga makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Ofisi za CCM, Wilaya ya Uyui ambao walikuwa wakifanya mkutano wa kawaida hasa Madiwani wa chama hicho ambao walikuwa wakijiandaa na kikao cha Baraza la Madiwani la Wilaya.


Taarifa hizo, zimebainisha kuwa, DC huyo alimuomba Rais John Pombe Magufuli kuwa anaachana na nafasi hiyo kwa ajili ya kwenda kufanya majukumu yake mengine.

Bw.Gabriel Mnyele hakuwa tayari kuelezea maamuzi aliyochukua na kuwataka Waandishi waliokuwa wakihoji hatua ya maamuzi yake wasubiri tamko kutoka juu.”Mimi sina la kusema kuhusu hilo nimeamua mwenyewe,kwani mmesikia kuwa nimetumbuliwa?Aliwahoji waandishi.

Mkuu wa Wilaya, Gabriel Simon Mnyele alikuwa miongoni mwa Wakuu wa Wilaya 139 walioteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 26 Juni, 2016.