RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SIMU AMBAZO HAZITAKUWA NA HUDUMA YA WHATSAPP KUANZIA JUNE 30 2017

Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma ya Whatsapp imesema kuna baaadhi ya simu za zamani zikiwemo zile zinazotumia mfumo wa Windows Phone 7.1, Android 2.2 na simu aina ya iPhone 3GS/iOS hazitakuwa na huduma za whatsapp kwa sababu wanataka kuendana na mifumo inayotumiwa na watu wengi.

Hatua hiyo ilitangazwa na Facebook mapema ya mwezi february mwaka 2016 ambapo huduma ya whatsapp ilitakiwa kuacha kazi katika mifumo hiyo ya programu mwishoni mwa Desemba 2016 na ilikuwa imeorodhesha simu za BlackBerry OS, BlackBerry 10, Nokia S40 na Nokia Symbian S60 kuwa miongoni mwa simu ambazo zingekatiwa huduma mwishoni mwa mwaka 2016 lakini ikabadilisha uamuzi wake na kuongeza muda hadi Juni 30, 2017.

Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia hivyo imeshauri wanaotumia simu za aina hiyo kununua simu za kisasa zaidi.