MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

WAFUGAJI WALIVYOKAA SIKU 7 PORI LA SELOUS WAKILA KINYESI CHA NG’OMBE, DAMU MKOJO


Gazeti la Habari leo limeripoti kuwa watu 50 wakiwa na watoto wamenusurika kufa baada ya kupotea ndani ya pori la akiba la Selous kwa siku saba, huku wakikosa chakula na maji na kulazimika kula kinyesi cha ngo’mbe, damu na mikojo ya binadamu.

watu hao ni wafugaji walikuwa wakihama na mifugo yao inayokadiriwa kufikia 1,780 kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Rufiji mkoani Pwani yakiwemo Chumvi na Muhoro wakielekea Morogoro ambako wanadai ndiko kuna makazi yao.

Wafugaji hao wanasema walitembea kwa siku tano ndani ya pori hilo, wakitarajia kufika Malinyi, yaliko makazi yao lakini hali ilikuwa tofauti, baada ya mwenyeji wao kuwalaghai kwa kuwapitisha njia zisizo sahihi. 

Wanasema waliishiwa chakula na maji ya akiba na mwisho walijikuta wanatokea pori la akiba la Selous; huku hali zao zikiwa zimedhoofu kutokana na njaa na kiu cha maji, pale walipoishiwa chakula na maji iliwalazimu kuanza kuchinja ng’ombe na kunywa damu kwa ajili ya kukata kiu pia walikula kinyesi cha ng’ombe ili kupunguza njaa.

Yule mwenyeji wao aliwatelekeza baada ya kuona hali zao zimekuwa mbaya, alitokomea kusikojulikana, akiwaacha wasijue pa kwenda, hivyo kulazimika kutelekeza mifugo yao ili kunusuru kwanza maisha yao.

Kiongozi wao anasema baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya alitafuta eneo lenye mtandao wa simu na kufanya mawasiliano mbalimbali na kuomba msaada.