RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

19.02.2017: MCH. NOAH LUKUMAY AHUBIRI JUU YA WATU KUTOKA KATIKA UTUMWA WA MATESO KATIKA IBADA YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

UJARI NA KUUTHAMINI WOKOVU WAKO KULIKO MALI NA MAGARI YAKO.

Katika ibada ya KUWATOA WATU UTUMWANI iliyofanyika Jumapili 19.02.2017 Mlima wa Moto Mikocheni “B”, Mch. Noah Lukumay alikuwa na haya ya kusema, “Kila mtu wakati anatembea anapaswa kutembea na Mungu na akiongea aongea na Mungu na mwisho wa siku aonekane katika maisha yake, afya yake. Tunapaswa kuepuke na magonjwa nyemelezi, magonjwa yanayoleta hasira kwenyi mioyo yetu. Naomba usema hivi, “Katika jina la Yesu tuko kinyume na roho ya magonjwa, roho ya kuonewa, kila utumwa wa magonjwa, leo tunaukomesha, kila ugonjwa sugu usio sikia dawa, leo tuko kinyume na ugonjwa wa preasure, kisukari, moyo. Leo tunakung’oa kwa jina ala Yesu, kila ugonjwa wa kichwa usiosikia dawa leo tunakuharibu kwa jina la Yesu.” Sema, “Katika jina la Yesu, kila ugonjwa unaorushwa juu ya kichwa, leo naita Damu ya Yesu kwenye utosi wa kichwa changu hadi unyayo wa miguu yangu, katika jina la Yesu. Kila mlango wa magonjwa, madeni, roho ya kukataliwa leo ninaufunga kwa jina la Yesu. Ee Bwana Yesu shuka juu yangu kwa ishara na maajabu katika jina la Yesu Amen. Waebrania 2:3 anasema, ”Sisi Je, Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kishaukathibitika kwetu na wale waliosikia. Ujari wokovu huu kwani wapo wengi wanakimbilia kwenye mafanikio, miujiza lakini wokovu wameacha mbali, wanatafuta habari ya kuambiwa mambo ya kesho na kesho kutwa mambo ya familia yake lakini mambo yake mwenyewe hataki. Wokovu wako ni wathamani kuliko magari, kuliko chochote ulicho nacho, unajua tunaacha dunia tutaacha na vitu vyake lakini tunaenda mbinguni na maisha yako utayaona mbinguni, maandiko yanasema, “Kila mtu atatoa hesabu ya maisha yake, ya kazi ya mikono yake.” Maandiko yanasema, “Kila kazi itapimwa kwa moto ikiteketea.” Amua sasa kumtumikia Mungu.

TENGENEZA MAISHA YAKO KWANI HUJUI NI LINI UTAKUFA
Bishop Dr. Gertrude amekuwa akihubiri maneno yenye nguvu ambayo yanakufanya uishi katika utakatifu. nachotaka kusema kwani ni kwamba, tengeneza maisha yako haujui ni lini utakufa. Tamaa na pesa unayoiendekeza kuliko kuendekeza Mungu, haitakukumbusha kumtafuta Mungu na ufalme wake. Unpotafuta kuwa na marafiki na watu wengi ujue unatafuta matatizo mengi. Sema, “Kuanzia leo nimeamua kubadilika na kuacha njia zote za shetani kwa jina la Yesu. Ee Bwana Yesu nauvua utu wa kale, utu wa dhambi kwa jina la Yesu Amen.” Kimbia dhambi kwani Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ametuambia kuwa mtu unakuwa humsalimie mwenzake na wengine wanasalimiana bila kuongea. Tu Tunapaswa kuwa mwili mmoja, tunapaswa kuwa watoto wa mama mmoja maana yake mkoba huwezi kuubana na bega lazima uelemewe. Kwahiyo tuelewane, mwambie tusigombane, katika maisha ya sasa utaona vitu vya kushangaza, utaona katika nyumba ya Mungu, watoto wa Mungu tu ndio wanaogombana wakati watoto wa shetani wala hawagombani, hawasengenyani lakini wana wa Mungu ndio wanaopigana. Naomba useme, “Kwa jina la Yesu kila utumwa leo ni mwisho, ewe shetani umenitumikisha yatosha kwa jina la Yesu.” Weka mkono wako kichwani sema, “Kuanzia sasa kila gonjwa la utumwa ambao umekaa juu yangu hauta kuwa na nafasi tena katika jina ala Yesu kila utumwa wa madeni ambao umenishikilia leo utengwe na mimi kwa jina la Yesu kila utumwa wa uharibifu kwenye kazi yangu achia kwa jina la Yesu, kila hasara inayo zaliwa katika maisha yangu leo ni mwisho kwa jina la Yesu kuanzia sasa Ee Bwana Yesu husika na maisha yangu, tokomeza roho ya utumwa popote ilipozaliwa kwa familia yangu, kwa watoto wangu leo ninaangamiza ninanyoa mizizi ya utumwa kwa jina la Yesu utoke kwenye roho ya utumwa. Amen. Sasa ndugu yangu tambua kuna kifo baada ya maisha haya. 

WATU MPO KWENYE UTUMWA NA HAMJIELEWI KABISA KWAMBA MNATUMIKISHWA
Watu wengine mpo kwenye utumwa wa mahusiano, hujijui lakini wewe ni mtumwa wa mahusiano, yaani wewe unakuwa saa zote unatumikia shetani na hiyo ni roho ambayo ipo kwenye familia yenu, kwenye ukoo wenu. Simama kwa miguu yako na uweze kufanya maombi. Kwa wale ambao wapo kwenye madeni na wanateseka, wanashindwa kulipa kwa sababu wametawaliwa na roho ya madeni na wengine roho hii inawafuatilia katika maisha yao. Watu hawa wamebaki ni utumwa kwenye kazi zao, kazi zao ziko level (hazipandi wala kushuka), hawapandishwi cheo, na ukiona hivyo ujue ni utumwa umewashikilia, sasa ni lazima tuingie ndani tuweze kuung’oa roho hizi chafu. Huwezi ukawa palepale katika maisha yako ni lazima uonyeshe kukuwa kimaendeleo na kifikra. Ni mtu gani asiyekuwa na hatua? Watu wanakuja wanakukuta upo palepale na wanakupita unabaki unajilaumu tu. Leo tunataka kushughulikia hiyo roho, haiwezekani ubaki kwenye utumwa inua mikono yako juu na tuombe, “Baba wa neema asante kwa watu hawa ambao naenda kuachilia, hivyo Bwana naomba ukaonekane juu yao, hakuna kama wewe. Ninaomba nyota yako na nguva zako ziende nao, wanapokuwa nyumbani wape kuonakana mbele zako katika jina la Yesu kristo. Kuna mtu ambaye yupo katika utumwa wa kutokuinuliwa kikazi, bosi wako hakuelewi, maneno kukushusha kazi yamekuandama, ya kudharauliwa, ya kutokueleweka, Bwana achilia nguvu zako juu yao katika jina la Yesu kristo, sema amen.