MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

19.02.2017: SEMINA KUBWA YA KARAKANA YA WANANDOA (MARRIAGE DINNER PARTY) KUFANYIKA 03.03.2017 MLIMA WA MOTO MIKOCHENI “B”

Siku ya Jumapili 19.02.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akishirikiana na kamati ya maandalizi ya Marriage Revival Dinner Party waliweza kuwahimiza watu kutoksa katika “KARAKANA YA WANANDOA” ambayo itafanyika siku ya Ijumaa 03.03.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” saa 12:30 jioni. Siku hiyo kutakuwa na mafundisho ya ndoa kutoka kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na walimu mbalimbali, maombezi, chakula na burudani. Kutakuwa na kiingilio kidogo sana, single wataweza kununua kadi kwa Tshs. 15,000/= na Double kwa Tshs. 30,000/=. Akiongea kwa msisitizo alisema kadi zinapatika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”, Kariakoo katika duka la Bahati Bukuku, Makumbusho, Victoria Petrol station-DSM. Pia watu wanaweza kununua kadi kwa njia ya Tigo Pesa” 0715 200 035 au Airtel Money: 0683 444 040. Pia kutakuwa na waimbaji ambao ni Bahati Bukuku, Manesa Sanga na wengine wengi wataimba siku hiyo.


Mzee wa kanisa Mzee Mwakitalu alimshukuru Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kuweka siku hii maalum ambayo itasaidia watu kujikomboa katika changamoto wanazopitia katika ndoa, pia jinsi ya kuondokana na chanagamoto hizo na kuimaarisha ndoa ili zidumua. Alisema kuna hasara kubwa sana ya kutengana na mweza wako, lakini ukiijenga ndoa yako utafurahi amaisha ya ndoa. Kwahiyo umepata upendeleo huo na changamkia kupata kadi hizi mara moja.


Wewe ambaye hukubahatika kufika katika ibada hii ya KUONDOKA KWENYE UTUMWA tunakualika katika ibada ya Jumapili hii itakayoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa, utaona magari ya Mlima wa Moto Mikocheni “B” au utasikia watu wakisema “Kanisani kwa mama Rwakatare”. Mungu na akubariki sana.