MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

26.02.2017: WATU WENGI WAFUNGULIWA KATIKA IBADA YA KUFUNGULIWA MILANGO ILIYOFANYIKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Siku ya Jumapili 26.02.2017 katika ibada ya KUFUNGULIWA MILANGO YAKO iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na Mch. Noah Lukumay wakishirikiana na watumishiu wa Mungu waliweza kupata muda mzuri kwaajili ya kuwaombea watu kufunguliwa milango yao ya baraka, mafanikio na afya njema ambayo ilifungwa ana adui shetani kwa muda mrefu. Ibada hii ilikuwa ni ibada ya tofauti sana kutokana na uwepo wa Mungu na nguvu za Mungu zilizokuwa zikifanya kazi kwa watoto wake katika kipindi cha maombezi. Watu wengi walipokea Roho Mtakatifu ambaye alienda kutibua makazi ya mapepo na majini katika miili ya watu. Watu wengi sana walifikishwa madhabahuni baada ya kuguswa na nguvu za Mungu huku wakiwa wamebebwa hawajiwezi kabisa. 

Kuna watu walikuwa wamefungwa na roho chafu, roho za madeni, magonjwa, kukataliwa, kuonewa, kudharauliwa, kutopandishwa mishahara na vyeo n.k lakini baada ya maombezi Mungu aliweza kufungua milango kwa watu hawa na wiki hii wanakwenda kupokea yale yote ambayo Mungu aliwafanyia siku ya ibada hii. Hakika Mungu ni mwema na anazidi kuwatumia watumishi wake kwa kiwango cha tofauti sana. 

Tunakukaribisha katika ibda ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho hapa DSM au Mwenge kwenye mataa barabara ya Cocacol utasikia watu wakisema kanisa kwa Mama Rwakatare, ingia humo na baada ya ibada utarudishwa kituoni. Mungu akubariki sana.
 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare