RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

#GLOBALUPDATES: HATIMAYE! YOUTUBE KUJA NA HUDUMA YA KULIPIA BUNDLE LA TV


Mtandao ndio kila kitu siku hizi, kila linapotokea jambo huwa ni rahsi sana kulijua ama kuliona moja kwa moja kupitia mtandao, iwe live au recorded ushindani wa mtandao umekuwa mkubwa sana na ndio maana YouTube wameamua kujiongeza na kukusogezea hii mpya.

Kizazi cha mtandao kinazidi kuwa kikubwa licha ya kuwa bado kuna mamilioni ya watu duniani ambao bado wanapenda kutazama TV za kawaida (Traditional TV), mwenendo wa kibiashara hauwezi kulifumbia jicho kizazi hiki cha kidigitali na ndio maana YouTube imejipanga kuisogeza kwetu huduma ya Streaming TV kwenye viganja vya mikono yetu.

YouTube Streaming TV ni huduma itakayowalenga wale watu (The YouTube Generation) wanaopenda kuangalia kile wakitakacho, muda wowote wautakao, kwa njia yoyote waitakayo na mahali popote watakapo. Kwa mujibu wa blog yao, YouTube imetoa listi ya aina tofauti za chanels za ku-subscribe kwa kiasi cha bundle la $35 kwa mwezi ambayo ni sawa na shillingi 78,200/= za Kitanzania.

(Imetafsiriwa hapa chini)..

” Huduma ya YouTube TV itakuwezesha kulipia bundle ambalo litakuwa ni nusu ya kile unacholipia kupata huduma ya chanel zako pendwa kwenye kingamuzi cha kawaida, na wala haikulazimisha kuilipia kila mwezi. Malipo ya kujiunga na huduma hii ni $35 (Tzs.78,200) na unaweza kujiondoa kwenye huduma hii muda wowote“. – YouTube.

Hizi ni baadhi ya chanels zitakazokuwa zinapatikana kwenye huduma ya YouTube Streaming TV:


Hizi ni baadhi ya picha za muonekano wa jinsi vipindi tofauti vya YouTube TV vitakvyokuwa vinaonekana kwenye simu, TV, Laptop, iPad na Tablet nyingine.





Kwa bahati mbaya huduma hii haitakuja na chanel kama za MTV, BET, Comedy Central na nyinginezo zinazopendwa na watu wengi kutoka Africa, pia kwa mujibu wa mtandao wa The Verge, YouTube TV haitaweza kuonyesha chanel za habari kama CNN, TBS na AMC Networks.

Kwa taarifa zaidi tembelea blog yao hapa.

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.

SOURCE: GLOBAL PUBLISHER