Rulea Sanga ameshangazwa sana na mkono wa Mungu juu yake kwa kumtimizia lile Neno ambalo Bishop Dr. Gertrude Rwakatare amelisimamia kwa mwaka huu 2017 ambalo linasema, "Mwaka 2017 ni Mwaka wa Kukumbukwa na Bwana". Mungu ameweza kutimiza Neno hilo kwa kuweza kumkumbuka Rulea Sanga kwa kumpa shamba la eka 2 lililoko mbele ya Chanika katika kijiji cha Mwanzo Mgumu mkoani Pwani. Akiongea na Rumafrica, Rulea Sanga amesema kwa sasa anataka kujikita katika kilimo, kwani eneo alilopata linafaa sana kilimo cha mihogo, mpunga na mahindi kwahiyo anatarajia kulima mazao hayo na zoezi hilo limeshanaaza. Kwahiyo aliwaomba watumishi wa Mungu kuzidi kumuombea ili aweze kutimiza ndoto hiyo na kauli ya Rais Magufuli ya "Hapa Kazi Tu"
Rulea Sanga - Mwanzo Mgumu - Pwani
BAADA YA KUWEKA BICON NA KUANZA KULISAFISHA KWAAJILI YA KILLIMO
MPUNGA UKIWA UMEPANDWA 06.04.2017