RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

DKT. MWAKYEMBE ASHUHUDIA MV. RUVUMA IKIINGIZWA ZIWA NYASA KWA MAJARIBIO ITUNGI PORT, KYELA

Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na Mbunge wa Kyela jana Machi 1, 2017 ameshudia zoezi la kuingizwa majini kwa Meli mpya ya pili ya mizigo iitwayo MV Ruvuma kwenye bandari ya Itungi, Wilayani Kyela, mkoa wa Mbeya. 
Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba mzigo zaidi ya tani 1000 inaungana na Meli nyingine mpya MV Njombe yenye uwezo wa kubeba tani kama hizo ambayo iliingizwa majini siku tano zilizopita. Meli zote mbili zipo kwenye hatua ya mwisho ya utengenezaji na majaribio kabla hazijaanza rasmi kazi ya kubeba mizigo kwenye ziwa Nyasa. 
Tayari wateja mbalimbali wamejitokeza kutaka mizigo yao ianze kubebwa na meli hizo mpya, yakiwemo makampuni yanayojishughulisha na biashara ya makaa ya mawe.
Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na Mbunge wa Kyela (shati la buluu) akishuhudia MV Ruvuma ikitelemshwa majini kwenye cherezo ya bandari ya Itungi, Wilayani Kyela, mkoa wa Mbeya.

Wananchi wakishuhudia MV Ruvuma ikitelemshwa majini kwenye cherezo ya bandari ya Itungi, Wilayani Kyela, mkoa wa Mbeya.

Wananchi wakishuhudia MV Ruvuma ikitelemshwa majini kwenye cherezo ya bandari ya Itungi, Wilayani Kyela, mkoa wa Mbeya.