RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MADAKTARI BINGWA WA INDIA WAFANYA UPASUAJI WA WAGOJWA MUHIMBILI DAR.


MADAKTARI Bingwa sita kutoka Hospitali ya Saifee nchini India wamefanya upasuaji wa wagojwa 12 waliokuwa wamelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kufanyiwa matibabu.

Waarabu na madaktari bingwa kutoka nchini India.

Madaktari hao wamekuja hapa nchini kutokana na ujio wa Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtakatifu Dkt. Syedna Alqadr baada ya kufanya ziara yake hapa nchini mwaka Jana Oktoba.


Mgonjwa akielezea namna alivyofanyiwa upasuaji na anavyoendelea hivi sasa.

Wakati akimalizia ziara yake alikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na kumuahidi kuleta madaktari wa moyo nchini ambao watashirikiana na madaktari wa taasisi hiyo ambao na wao wamepokea ujio huo kama njia mojawapo iliyowapatia ujuzi wa elimu kuhusiana na masuala ya upasuaji ya mishipa na moyo.

Aliyesimama ni daktari bingwa wa upasuaji mishipa ya damu hapa nchini, Dkt. Bashir Nyangasa.



Na Denis Mtima/GPL