RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRIKAUPDATES: WHATSAPP WALETA UPDATE MPYA INAYOFANANA NA ‘SNAPCHAT STORIES’.



Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa Snapchat na Instagram stories basi nina imani utaenjoy update mpya ya ‘WhatsApp status.’

Ushindanni wa social media Apps unazidi kuwa mkubwa na WhatsApp ni miongoni mwa Apps zinazoongoza kuwa na watumiaji wengi sana. Kuelekea miaka minane ya WhatsApp tarehe 24 Februari 2017, WhatsApp wamekuja na feature mpya itakayomruhusu mtumiaji kusave status yake kwa kutumia picha au video.
Hii ipoje? Na inafanya kazi vipi?

Kama vile ilivyo Snapchat na Instagram Stories, WhatsApp itaanza kukuwezesha kupost na kushare‘Stories’ na kisha kuiweka story yako (picha au video) kwenye status yako ambapo mtu yoyote aliye kwenye contacts zako na anaetumia WhatsApp ataweza kuiona picha au video hiyo kwa masaa 24 kabla haijapotea.


Kingine kizuri kuhusu update hii ni kwamba mtu anaweza kujibu status updates hizo moja kwa moja kutoka kwenye WhatsApp stories. Unaweza pia ukachagua nani aone au asione kile ulichoki-share kwenye status/story yako kwa kuziseti ‘privacy settings’ zako za WhatsApp.

Jinsi ya Kuweka/ Kutumia WhatsApp Status Mpya:

Kujifunza namna ya kutumia WhatsApp status feature mpya, fuata njia zifuatazo hapa chini.
Fungua WhatsApp yako kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa ‘Status’ juu ya screen yako.
Kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa ‘My status’, sehemu hii inakiduara cha kijani yenye alama ya nyeupe ya +.
Ukisha fika hapo utakuwa na uwezo wa kuchukua picha, kurekodi video au ku-upload picha au video ambazo zipo kwenye gallery yako tayari.
Hatua inayofuata ni kuiedit/kuipamba, kuiwekea emoji, ama kuweka maandishi kwenye picha au video yako. 
Ukimaliza kufanya vyote hivyo, bonyeza ‘Send’ na status/story yako itakuwa hewani.

Update feature hii imeanza kupatikana kwanzia jana kwa watumiaji wote wa Android, iPhone na Windows Phone.

Update your WhatsApp and enjoy!