RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SERIKALI YANUNUA MTAMBO WA KISASA WA KUTAMBUA DNA, DAWA ZA KULEVYA, SUMU NA MADINI


SERIKALI kupitia Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imenunua mtambo mpya na wa kisasa wa aina ya Energy Dispersive X Ray Fluorescence (EDXRF) Kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa kimaabara wa kutambua aina na kiasi cha madini (metals) kwenye sampuli husika.


Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele (katikati) akizungumza na wanahabari. 

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake, Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele amesema kuwa mtambo huo utaweza kufanya utambuzi wa uchunguzi wa makosa ya jinai kama vile sampuli za vinasaba (DNA), dawa za kulevya, sampuli za sumu na nyinginezo Kwa haraka sana ili kutoa majibu yanayowezesha utoaji wa haki katika vyombo vya sheria.


“Mtambo huu tumeusimika kuanzia Februari 21 na 23 mwaka huu katika Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mkoani Mbeya.” Alisema Prof Manyele.


Wanahabari wakifuatilia tukio hilo.