RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MH. BISHO DR. GERTRUDE RWAKATARE ALIVYOIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA KUTEULIWA KWAKE NA JUU YA PASAKA

EXCLUSIVE: MH. BISHOP DR. GERTRUDE ALIVYOONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU SIKU MAALUMYA PASAKA 2017 SIKU YA JPILI 16.04.2017


Tukiwa tunasherekea Pasaka ya sikukuu ya Ufufuo wa Kristo, na ni mwaka mpya wa Kiroho kwa Wakristo ambapo tunatafakari mwaka jana ulishindwa nini? Pengine ulikuwa unatoa sana, au unaabudu sana, ulikuwa unahuzulia ibada sana na badae ukaacha. Inapofika mwaka mpya lazima ufufuke na Kristo, unapofufuka maana yake unanza upya, kwahiyo hudhuria ibada kanisani, soma Bibilia, toa kwa wingi ukijua unamtolea Mungu, watembelee watu wenye shida, tutiane moyo kwa maana Pasaka ni upendo. Katika Pasaka Yesu alitimiza Neno la Mungu linalosema, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu akamtoa mwanaye wa pekee ili kila mtu aokoke”, kwahiyo Yesu alikufa kwa ajili yetu ili tuokoke, Yesu alitesa, alipigwa msalabani kwa ajili yetu na kwa kupigwa kwake sisi tumepona, kwahivyo basi ninawasihi wote, ninawaomba tuanze kupendana, tuanze upya kuchukuliana, Pasaka siyo sherehe ya chakula, wala siyo sharehe ya kulewa pombe, basi tutembeleane, tumpende Mungu na ndugu zetu.


MH. BISHOP DR. GERTRUDE ALIVYOONGEA NA WAANDISHI
WA HABARI KUHUSU KUTEULIWA KUWA MBUNGE KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI

Ningependa kumshukuru Mungu kwa kipindi hiki cha Pasaka kwaajili ya uteuzi kuwa mbunge wa viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi. Rais wetu Dr. John Pombe Magufuli ameniteuwa nirudi tena Bungeni, ninamshukuru Mungu sana kwaajili ya busara zake na kwa ajili ya wema wake, Yeye ni mtenda haki na amenikumbuka kama wana Mlima wa Moto tunavyosema mwaka huu ni MWAKA WA KUKUMBUKWA. 
Nilikuwa nasikia wengi wakiteuliwa lakini leo na mimi nimekumbukwa pasaka hii cheo changu kimefufuka na Kristo narudi tena Bungeni namshukuru Mungu, namshukuru Rais wetu, nashukuru chama changu cha Mapinduzi, nashukuru na wote waliokuwa nyuma yake wakimsaidia, wakimshauri. BWANA asifiwe! Tunatakiwa tumuombee Rais wetu katika uongozi wake huu Mungu amlinde, amtetee, Mungu ampiganie, Mungu ambariki Rais wetu.

 Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akipokea zawadi kutoka kwa muumini wake
  Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akipongezwa na Mh. Mary Mwanjelwa