MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

14.05.2017: SIKU YA MAOTHER'S DAY WATU WENGI SANA WALIOKOA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuokoa roho za watu siku ya Jumapili ya Mother's Day tarehe 14.05.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikochemi "B". Watu wengi sana waliweza kujitokeza katika ibada kuombea wamama dunani na kuamua kuchukua uamuzi wa kuokoka na kumpokea Yesu Kristo kuwa BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAO.

Mch. Elizabeth Lucas aliweza kuwaongoza sala ya toba na kuwaombea akishirikiana na jopo la wachungaji na waumini wote wa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Baada ya kuongozwa sala ya toba na kufanyiwa maombezi, wangofu wapya waliweza kubatizwa na siku ya Jumatatu na Jumanne wataingia katika darasa la kukulia wokovu.

Kipindi cha maombezi baadhi ya waongofu wapya walitokwa na guvu za giza na wengine wakijikuta wanagalagala chini baada ya kuguswa na NGUVU za MUNGU zilizokuwa zinapigana na roho chafu za kuzimu zilizokuwa zikiwatesa kwa muda mrefu.

Ndugu zetu hawa wanahitaji sana maombi yako ili wazidi kudumu katika wokovu. Kipindi hiki ni kigumu kwao kwasababu shetani yuko vitani kuhakikisha watu hawa wanarudi nyuma katika wokovu.

Kumbuka na wewe wakati unaokoka kuna watu waliomba kwaajili yako na ndio maana unazidi kusonga mbele katika wokovu. Na hawa ndugu zetu wanahitaji sana maombi yako ili wadumu katika wokovu.

Wewe ambaye bado hujaokoka, nafasi bado zipo, mlango wa Mungu uko wazi, amua sasa kuokoka, usingalie ndugu na jamaa watasema nini, muangalie Yesu Kristo, angalia maisha yako. Hakuna mtu anajua ni jambo gani litamtokea hapo baadae, kwahiyo yaandae maisha yako ya baadae baada ya kutoka hapa duniani.

Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na katikati ya wiki ibada inaanza saa 9 mchana hadi saa 1 jioni. Mungu akubariki sana na akupe ujasiri wa kuchukua uamuzi wa kuokoka sasa.
Mch. Elizabeth Lucas