MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE: TAFAKARI YALE AMBAYO MUNGU AMEKUTENDEA!

Mungu amekuepusha na mengi tangia ulipoamuka kitandani kwako. Kuna mambo mengi mabaya yametokea lakini Mungu amekuvusha nayo. Hata kama wewe uko kitandani unaumwa ila kuna mambo mengi mabaya ambayo Mungu amekuepusha nayo, yawezekana ikawa ni matatizo katika familia yako, kazi yako, miradi yako, ndoa yako, ajira yako, mifugo yako, mazao yako, elimu yako, malengo yako n.k.
Inawezekana wewe unapitia changamoto fulani lakini bado Mungu amekuepusha na mabaya ambayo ni makubwa kuliko hiyo changamoto unayopitia.

Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Sasa naomba uchukuie dakika chache umshukuru Mungu kwa kuepusha na hayo mabaya yaliyowatokea wengine siku ya leo.

Kuna watu wengine wamewekewa UTASA katika maisha yao, kila wanachofanya HAKIZAI. Shetani ameshika milango ya mafanikio ya watu, kila wakijitahidi kufanya kazi kwa bidii hawaoni MAFANIKIO, pesa wanayopata ni kwaajili ya kula tu. Inaumiza sana kuona watu hawa wanateseka.

Sasa kwa kuyaona hayo mateso ya watu hawa, Mungu wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" ametupa maono ambayo TUNAAMINI yatabadilisha maisha ya watu kwa kiwango cha juu sana. Jumapili hii 04.06.2017 saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana tutakuwa na MAOMBI YA KUVUNJA UTASA WA MAISHA YAKO NA AFYA YAKO, kwahiyo unatakiwa kuwahi mapema ukiwa na TUNDA LAKO lolote lile. Mungu atafanya kitu kupitia tunda lako. NINAOMBA USOME Yohana 15:16.

Acha kujiuliza itakuwaje? Njoo ukiwa na IMANI kuwa YESU MTENDA MIUJIZA atafanya jambo katika maisha yako. MUNGU AKUPE UJASIRI WA KUHUDHURIA IBADA HII YA AINA YAKE. Ubarikiwe na BWANA..

Usafiri ni bure kwenda kanisani na kurudi kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, utasikia watu wakisema kanisa kwa mama Bishop Gertrude Rwakatare

//Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare//
//Mlima wa Moto Mikocheni "B"//
//USIKOSE KUFIKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" JUMAPILI HII//