RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Watoto Walionusurika Ajali Karatu, Kuagwa Jumapili Kwenda Marekani


ARUSHA: Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema kuwa, tayari ndege aina ya DC 8 imepatikana ambayo itawasafirisha watoto watatu walionusurika kwenye ajali ya gari Karatu kwenda kutibiwa nchini Marekani mpaka pale watakapopona.

Nyalandu amezungumza hayo leo na wanahabari jijini Arusha na kueleza kuwa ndege hiyo inatarajiwa kuwasili leo Jumamosi, katika Uwanja wa Ndege wa KIA na hafla ya kuwaaga itafamyika Jumapili.


Kupitia Instagram na Twitter, Nyalandu ameandika:

“Ndege aina ya DC 8, itakayotumika kama ‘air ambulance’ inatarajiwa kuwasili Kilimanjaro kesho Jumamosi, Mei 13 ikitokea Charlotte NC tayari kwa kuwachukua watoto wetu kwenda kutibiwa zaidi katika hospitali ya Mercy, Sioux City IA.”

“Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ataongoza hafla ya kuwaaga watoto watakaosafiri kwenda nje kwa matibabu siku ya Jumapili, kutokea KIA.”

Ajali hiyo ilitokea Jumamosi iliyopita na kusababisha vifo vya watoto (wanafunzi) 32, walimu wawili na dereva wao.


VIDEO: Eneo la Ajali Mazito Yaibuka Karatu, Viongozi wa Kijiji, Madereva Wanena