MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

18.06.2017: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AMPONGEZA RAIS MAGUFULI NA MCH. MZEE WA UPAKO AKUBALI KUSAIDIWA MIL. 1 NA BISHOP DR. RWAKATARE

Siku ya Jumapili 18.06.2017 Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na Mch. Noah Lukumay wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliweza kufika katika ofis za CLOUDS TV na kuweza kuzungumza machache na watangazaji wa kipindi cha CHOMOZA ambao ni Uncle Jimmy na Sam Sasali kuhusiana na maombezi ya kuliombea Taifa la Tanzania, rais wa Tanzania, Bunge la Tanzania na Jeshi la Ulinzi.

Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare  alikuwa na haya ya kusema, Bwana Yesu Apewe Sifa! Binafsi ninamshukuru sana Rais John Pombe Magufuli  kwa kazi alizozifanya kwa kipindi kifupi tangia ameingia madarakani  kwa kuvumbua wafanyakazi hewa, madawa ya kulevya, makontena kwani ufisadi ulikuwa mkubwa sana, pembe za ndovu, matatizo ya dhahabu. Jamani lazima tumuombee Raise wetu na kumpongeza. Huyu mtu ni kama ameshika masharubu ya simba, na ndio maana kila wakati anasema, "Jamani niombee watu wa Mungu" kwasababu anajua ili afanikiwe anahitaji mkono wa Mungu.

Nasi tunaomba Jeshi la Mungu limlinde, malaika wamzunguke, wigo wa moto wa Roho Mtakatifu umzunguke. Wenye nia mbaya basi mashimo waliochimba yawadondokee wenyewe.

Rais wetu ni zawadi yetu kutoka kwa Mungu, yaani ni bidhaa adimu, anakana uhai wake kwaajili ya watu wengine, anajitoa kufanya kazi kwa bidii kutoka ndani ya moyo wake kuwahudumia matajiri na masikini. 

Sasa basi  kama una zawadi yoyote au maua au tuzo mpelekee sasa kwa kumpongeza kwa kazi nzuri alizofanya. Jamani mpe mtu maua wakati bado mzima na sio kumpa maua wakati amekufa, na ukifanya hivyo utamtia moyo Rais wetu

Mch. Noah Lukumay naye alikuwa na haya ya kusema, Nasi kama wana Mlima wa Moto Mikocheni "B" tunamuombea azidi kuwa na hekima na maarifa. Tumeona kwa muda mfupi ameweza kuvumbua vitu ambavyo vilikuwa havijulikana, na hii ni hekima na maarifa ambayo Mungu ameweka ndani yake. Rais wetu ana hekima ya ziada na sio ya shule ila ni hekima ya Mungu na ndio inayofanya kazi. Kwahiyo basi tunaomba tuzidi kumuomba Mungu ili Rais wetu azidi kuwa na hekima, afya na ulinzi ili azidi kulitumikia Taifa letu la Tanzania.

Pia Mchungaji Anthony Lusekelo (Mzee Wa Upako) alimshukuru sana Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kuwa ni Mchungaji pekee wa kwanza kumsaidia milioni moja (1,000,000/=) na kumwambia asonge mbele kwani mke mzuri, gari zuri maisha mazuri atayapata kwa kuhubiri INJILI

Baada ya kumaliza mahojiano aliweza kuelekea kanisani kwaajili ya ibada maalum ya kuliombea TAIFA LA TANZANIA.

Endelea kufuatilia post zetu kujua kile alichokihubiri siku ya Jumapili Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Chanzo Cha Habara: Mlima wa Moto Online Magazine.