RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

25.06.2017: WATU WAZIDI KUOKOKA NA KUMPOKEA YESU KRISTO KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" KAMA UNAVYOONA HAWA WALIOKOKA JUMAPILI

Bwana Yesu apewe sifa mwana wa Mungu. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kibali alichotupa kuiona siku ya leo. Mungu ni mwema, kwani kuna watu walitamani kuiona siku ya leo lakini haikuwezekana. Kuna watu walitamani kuokoka lakini walishindwa kupata nafasi ya kuokoka na wakapoteza maisha yao kwa ugonjwa, ajali, kupigwa risasi, kulogwa n.k. Mungu amekuwa mwammini kwetu sisi ambao bado tunazidi kuishi na tunafurahia uzima aliotupa Mungu wetu wa mbinguni.

Siku ya Jumapili 25.06.2017 watu wengi waliweza KUOKOKA katika ibada ya KUONDOA NJAA Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Mch. Francis Machichi na Mch. Noah Lukumay waliweza kuwaongoza sala ya toba, kuwaombea na kuwabatiza kwa maji mengi.

Siku ya Jumatatu na Jumanne wataanza masomo yao ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 10 jioni.

Ni wajibu wetu wa kuwaombea hawa ndugu zetu ili wazidi kudumu katika wokovu. Kipindi hiki ni kipindi cha vita dhidi yao kwani shetani anafanya kila njia kuwarudisha nyuma. Ila nina amini maombi yako yatasababisha watu hawa kusonga mbele katika wokovu. Wewe ni mtu wa muhimu sana katika kuwaimarisha watu hawa wadumu katika wokovu kupitia maombi yako na pia kuwafundisha Meno la Mungu.

Kumbuka hata wewe siku uliyookoka kuna watu walitumia muda wao kukuombea udumu katika wokovu na ndio maana mpaka leo unafurahia maisha ya wokovu. Sasa imefika zamu yako ya kuwaombea hawa ndugu zetu ili wazidi kumtumikia Mungu kama unavyomtumikia wewe. Wameteseka na maisha ya dhiki na taabu wakiwa chini ya himaya ya shetani kwa kipindi kirefu, na ndio maana siku ya leo wameamua kumkimbia shetani na kuja kwa Mungu ili maisha yao yabadilike na siku ya mwisho wamkamuone Mungu mbinguni.

Ikiwezekana simamisha kazi unayofanya sasa hivi na anza kuwaombea hawa watoto wa Mungu. Tamka ulinzi juu yao, mafanikio katika maisha yao, bidii ya kumtumainia Mungu, hamu ya kusoma Neno la Mungu, hamu ya kutamani kufika kanisani, hamu ya kuwa watoaji, hamu ya kutii maagizo ya wachungaji wao, tabia ya kuungama dhambi zao wanapokosea na mengine mazuri juu yao.

Mungu akubariki sana, naami utayafanya haya kwaajili ya utukufu wa Mungu.

Na wewe ambaye ulitamani kuokoka, nafasi bado unayo. Jitahidi Jumapili hii kufika katika ibada ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" saa 3 asubuhi, na ukiona Jumapili ni mbali njoo katikati ya wiki saa 10 jioni utakutana na watumishi wa Mungu, watakuongoza sala ya toba na kukuombea.

Nikutakie siku njema na yenye mafanikio. Amen

//Bishop Dr. Gertrude Rwakatare//
//Mlima wa Moto Mikocheni "B"-Dar es Salaam Tanzania//
//Ibada Jumapili ni saa 3 asubuhi - saa 8 mchana//
//Usafir ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho -DSM au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola utaona magari yetu//