MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

25.06.2017: MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ALIVYOWASIMIKA RASMI WAINJILISTI WAPYA KWAAJILI YA HUDUMA YA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare katika ibada ya maombi ya KUONDOA NJAA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 25.06.2017 aliweza kuwasimika wainjilisti wapya watakaofanya kazi ya Mungu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakishirikiana na wachungaji kwaajili ya kuhubiri Injili mitaani na kanisani, kuwaleta watu kwa Yesu.

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akishirikina na wachungaji wa kanisa hilo waliweza kuwaombea na kuwatamkia maneno ya baraka kwaajili ya kazi ya Mungu. 

Pia Bishop Gertrude Rwakatare aliwashukuru kwa kukubali kufanya kazi ya Mungu pamoja naye wakiwa bado vijana kabisa na wenye nguvu. Kanisa zima liliweza kuwaombea wainjilisti hawa na kuwakabidhi mikononi mwa Mungu kwaajili ya kuanza kuchapa kazi ya Mungu.

Nasi kama wafuasi wa Mungu, tunahitaji sana kuwaombea watumishi wa Mungu hawa ili wazidi kusonga mbele kwa kazi ya Mungu. Tuwaombee maisha yao yakawe ya baraka amani na furaha, kila watakalofanya kwa utukufu wa Mungu likalete majibu. Watu wakapokee uponyaji na kufunguliwa kupitia vinywa vyao, wakafanye kazi ya Mungu kwa uaminifu. Mungu azidi kuwapigania na kuwainua kimwili na kiroho ili wasirudi nyuma walikotoka.