RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Mwanasiasa wa muda mrefu Kenya GG Kariuki afariki dunia



Mwanasiasa wa muda mrefu Kenya, Godfrey Gitahi Kariuki, maarufu kama GG Kariuki amefariki dunia.

Bw Kariuki amekuwa seneta wa jimbo la Laikipia mashariki mwa mji mkuu wa Nairobi.

Seneta Kariuki alikuwa ndiye mbunge pekee aliyekuwa katika bunge la wakati wa uhuru Kenya ambaye alikuwa bado mbunge.

Alichaguliwa mara ya kwanza bungeni Mei 1963 na akahudumu kama mbunge mfululizo kwa miaka 20 kabla ya kupoteza kiti katika uchaguzi wa 1983.

Alihudumu mihula kadha kama mbunge wa eneo bunge la Laikipia Magharibi na alihudumu kama waziri serikali za Mzee Jomo Kenyatta na Daniel arap Moi.

Rais Uhuru Kenyatta ametuma salamu za rambirambi na kumweleza Bw Kariuki kama kiongozi aliyechangia katika ukombozi na ukuaji wa Kenya kama taifa.
Bw Kenya amesema licha ya umri wake aliendelea kuchangia siasa na mustakabali wa taifa na alikuwa na usemi wa busara wakati wa mizozo na majibizano kuhusu masuala ya kitaifa.
"Alichangia katika kutatua mizozo ya maskwota, hasa Laikipia na pia alitetea haki za Wakenya wote alipohisi kwamba zinakandamizwa na waliokuwa mamlakani," Rais Kenyatta amesema.