MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

02.07.2017: MAMA ALIYEPAGAWA NA MAPEPO AOMBEWA NA BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Siku ya Jumapili 02.07.2017 ikiwa ni siku ya kwanza ya semina ya MID YEAR CROSS OVER 2017 mama mmoja ambaye alikuwa akisumbuliwa na mapepo kwa muda mrefu aliweza kufika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwaajili ya maombezi. Akiwa kanisani hapo, Mch. Noah Lukumay aliweza kuwaombea watu wenye kusumbuliwa na mapepo na shida mbalimbali, wakati akifanya maombezi aliweza kumtaja mama aliyekuwa akisumbuliwa na mapepo, naomba apite mbele. Mama huyu baada ya kusikia sauti hiyo mara moja alipiga kelele na kuanza kugalagala chini huku akisumbua wahudumu waliofika kuksaidia kumpeleka madhabahuni. Baada ya kufikishwa madhabahuni Bishop aliweza kumuombea na mapepo kwa nguvu za Mungu yakamtoka mara moja. Mama huyu na mume wake walielekea katika eneo lao wakamshukuru Mungu.

yawezekana na wewe una mapepo au majini na yanakusumbua kwa muda mrefu. Usikose semina hii ya KUVUNJAVUNJA KAZI ZA SHETANI zilizosababisha maendeleo yetu kurudi nyuma, na pia kufunga milango ya shetani katika maisha yetu na kazi zetu kwa miezi sita iliyobaki kumaliza mwaka 2017. Tunajua ya kuwa mambo yaliyombele yetu ni GIZA NENE, hatujui ni jambo gani litatukumba. Kwahiyo unayo nafasi ya kuhudhuria semina hii ambapo tutamkabidhi Mungu wetu maisha yetu ili yawe na ulinzi wa KIMUNGU.0