RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

02.07.2017: MCH. DANIEL KALEGE AKONGA MIOYO YA WATU KATIKA SEMINA YA MID YEAR CROSS OVER 2017 INAYONDELEA KANISANI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Bwana apewe sifa!

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa siku ya Jumapili 02.07.2017 kwa upendeleo na kibali alichotupa Mungu kuiona hii. Wapo watu wengi sana hawakubahatika kuiona siku ya Jumapili hii na walitamani sana kuiona lakini walishindwa na wakatoweka dunani. 

Jumapili hii tumeona Mungu akiwatumia watumishi wake, Bishop dr. Gertrude Rwakatare, Bishop Dunstan Maboya na Mch. Daniel Kalege kutoka Uganda kuzindua rasmi semina ya siku 8 ya MID YEAR CROSS OVER 2017 ya kumshukuru Mungu kuvuka miezi sita tangia mwaka 2017 uanze na pia kumkabidhi Mungu maisha yetu kwa miezi sita ijayo ili iwe na ulinzi dhidi ya maadui zetu, miezi ya kuwa na mafanikio, miezi ya kuteketeza kazi za shetani, miezi ya kuvunja nguvu za wachawi, wabaya wetu, miezi ya kuondoa umaskini, ufukara, njaa, upweke wa kuishi bila mume wako au mke wako, ubachela, kukosa mume/mke, kukosa watoto, kukosa amani ndani ya familia na ndani ya ndoa, kukosa mali, kukosa fedha, kukosa viwanja na majumba, kukosa mafanikio, kukosa kazi, kukosa promosheni, kukosa ajira, kufeli masomo, kuondoa maonezi, kukosa wateja, kukosa mitaji, kuondoa hali ya kushindwa kumiliki mali zako, kuondoa madeni, kuvunja na kuziangamiza roho chafu na mengine kama hayo. 

Siku ya leo Mch. Daniel Kalenge kama anavyoonekana kwenye picha alitubariki na Neno la Mungu ambalo lilitugusa na kubalisha fikra zetu. Mungu alimtumia mtumishi huu kwa namna ya tofauti sana. Watu walionekana kubarikiwa kutoka na wingu la uwepo wa Mungu lilivyotanda katika kanisa hili la MLima wa Moto Mikocheni "B". Mchungaji huyu ametokea Uganda na atakuwepo katika semina hii kwa siku 8. Mungu amempa mzigo wa tofauti sana kwaajili ya watu wake. Kwahiyo usitamani kabisa kukosa semina hii ambayo imeanza Jumapili 02.07.2017 hadi Jumapili 09.07.2017. katikati ya wiki itaanza saa 9 mchana hadi saa 1 jioni na siku ya Jumapili itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. 

Nasi tupo katika maadalizi ya somo la Jumapili ambalo alilifundisha Mch. Daniel kalenge, kwahiyo endelea kufuatilia post zetu.






















































Comments