RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

02.07.2017: MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AWATAKA WATU KUTOWAKATISHA WATU TAMAA NA KUSABABISHA WAKASHINDWA KUJA KANISANI

Bwana apewe sifa! 
Katika siku ya kwanza ya Ufunguzi wa semina ya MID YEAR CROSS OVER 2017 (Semina ya kumshukuru Mungu kuvuka miezi sita na kumkabidhi Mungu maisha yetu miezi zita iliyobakiki kmaliza mwaka 2017). Tumeona ukuu wa Mungu kupitia watumishi wake. Watu wamefunguliwa na kupokea ujumbe ambao utawasaidia kwa miezi sita iliyobaki ya kumaliza mwaka. Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alihimiza watu kutokuwa na maneno ya uchonganishi na uzushi , fitna , usengenyaji, kuwakatisha watu wengine tamaa ya kuja kanisani, kuropoka maneno yasio na utukufu mbele za Mungu na mbele za watu, kutoa maneno yasio na maana. Ujumbe huu uligusa watu wengi sana kwani wengi wao wamekuwa wakikumbana na changamoto kama hizo na kusababisha kurudi nyuma kiimani na pengine kutofika kanisani.

Kama Wakristo tunahitaji kutiana moyo, unapoona mwenzako amekosea basi muonye na umuelekeze njia sahihi kuliko kutoa maneno mazito na pengine kumtukana mbele za watu. Unapoona mwenzako amekosea muite pembeni na umuelekeze naye atakuomba msamaha kuliko kuanza kuropoka maneno kanisani au kwenye madhabahu. Huu sio upendo bali ni chuki na Mungu hapendezwi kabisa. Ni lazima watu kuwa na hekima katika maneno tunayoyatoa kwa watu wengine. Kabla hujaropoka unatakiwa kutafakari na kumuuliza Roho Mtakatatifu akuongoze. Tabia hii mbaya imechangia sana watu kutopenda kuja kanisani. Nasi tunaikemea kwa Jina la Yesu.

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kupiga picha ya pamoja na wachungaji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Utukufu wa Jehovah!!

Bishop Dunstan Maboya na Mch. Daniel Kalege kutoka Uganda waliweza kufungua rasmi semina hii na kuikabidhi mikono mwa Mungu kwa siku 8 za semina hii ambayo itahitimishwa Jumapili 09.07.2017. Kwa siku za katikati ya wiki semina itaanza saa 9 alasiri hadi saa 1 usiku.

Yawezekana unapitia magumu na taabu, na umezunguka makanisa mbalimbali, kwa waganga kutafuta uponyaji lakini hujafanikiwa. Nataka kukuhimiza kutokosa semina hii ambayo itaongozwa na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Bishop Dunstan Maboya na Mch. Daniel Kalege kutoka Uganda. Ni siku 8 za kupokea BARAKA zako na kufunguliwa. Wajulishe na wenzako kwa "Ku-share" post hii au kwa njia yoyote ile unayoona kwako ni rahisi. Mungu anakuhitaji na anakupenda na ndio maana ameamua kuwatumia watumishi hawa kukusaidia. 










Comments