RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

02.07.2017: MUUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO KIGAMBONI NURUNI AKIMSHUKURU MUNGU KUSHIRIKI SEMINA YA MID YEAR CROSS OVER 2017 SIKU YA JUMAPILI

Neno la Mungu linasema, "Angalia umekuwa mtu mzima, usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililobaya zaidi" - Yphana 5:14

Tunaambiwa na Mungu tusitende dhambi na tukitenda tu basi jambo baya litakuja kwetu. Siku ya Jumapili 02.07.2017 ikiwa ni siku ya kwanza ya uzinduzi wa semina ya siku 8 ya "MID YEAR CROSS OVER 2017" uliofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ukiongozwa na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Bishop Dunstan Maboya na Mch. Daniel Kalege walimuomba Mungu na kumshukuru Mungu kwa kutufikisha miezi sita, na baadae walituombea ulinzi wa kulindwa na damu ya Yesu kwa miezi sita ijayo kumaliza Mwaka.
Katika ibada hii muumini na mzee wa kanisa la Mlima wa Moto Kigamboni Nuruni kwa Mch. Dickson aliweza kufika katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwaajili ya kumshukuru Mungu kwa kibali cha kuweza kuhudhuria semina hii ya tofauti. Mama huyu aliamini kwa kukanyaga eneo la kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", basi mambo yake yanakwenda kunyooka kwa miezi sita ijayo kumaliza mwaka 2017. Pia alimshukuru Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kuweka huduma ya Mlima wa Moto Kigamboni Nuruni, kwani kwa kipindi kirefu sana wamekuwa wakiteswa na wachawi na nguvu za giza, wakitumikishwa na watu wasiowajua kwa njia ya uchawi.
Yawezekana na wewe unapitia majaribu fulani na umejaribu kutafuta "solution" na hujapata majibu. Usikose kuhudhuria semina hii ambayo itahitimishwa Jumapili 09.07.2017 Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi. Na katikati ya wiki semina inaanza saa 9 mchana hadi saa 1 usiku. Semina hii ni semina ya kukabidhi maisha yetu kwa Mungu kwa miezi sita ijayo na kumshukuru Mungu kwa miezi sita iliyopita.




















Comments