MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

09.07.2017: DADA AMSHUKURU MUNGU KUAPATA SAFARI YA AFRIKA KUSINI

Siku ya JUmapili 09.07.2017 katika hitimisho la semina ya MID YEAR CROSS OVER lililofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, dada huyu alimshukuru Mungu kwa kumsafilisha salama katika safari yake ya Afrika Kusini. Amesema kabla hajaenda Afrika Kusini, alipopata taarifa kutoka kwa mkubwa wake wa kazi kuwa amechaguliwa kwenda Afrika Kusini hakuweza kuamini kutokana na taratibu za ofisini kwake jinsi zilivyo. Lakini alimshukuru Mungu kwa kupata nafasi hiyo, na pia aliamini maneno ya Bishop Dr. Rwakatare ambayo huwa mara nyingi akisema, "Pokea Safarai za nje ya Tanzania".
Yawezekana na wewe unatamani safari za Nje ya Tanzania kwajili ya masomo, kazi, biashara, kutembea, kula likizo, basi jiunganishe na upako wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na Mungu atakutendea. Ishi maisha ya IMANI utaona Mungu akifungua milango kwako,  mtumikie Mungu na ye atakusaidia, acha kutnda dhambi naye Mungu atakupigania, wapende watu wote naye Mungua atakupenda, yatii maagizo ya watumishi wake naye atayatekeleza mahitaji yako, uwe mtoaji naye atajitoa kwaajili yako, wasaidie wenye uhitaji naye atakusaidia utakapomhitaji.

Usikose ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.


0