RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

09.07.2017: MH. BISHOP DR. GERTRUDE ALIVYOYAOMBEA MAJI SIKU YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

// Nimekukimbilia wewe BWANA nisiaibike milele. Kwa haki yako niponye, uniopoe, unitegee sikio lako, uniokoe. Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, nitakapokwenda siku zoe-Zaburi 71:1-3 //

Siku ya Jumapili 09.07.2017 katika hitimisho la MID YEAR CROS OVER lililofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B kwa Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, waumini na wageni waliomkimbilia BWANA  ili wasiaibike milele katika  kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B waliweza kuombewa maji na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ili yafanyike baraka katika afya zao, mafanikio yao, biashara zao, kazi zao, mashamba yao, mifugo yao, amani katika ndoa zao, masomo yao, ajira zao n.k. Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliwaomba watu kuwa na imani kabla hawajatumia hayo maji kwani kila jambo la kiimani hufanyika kwa IMANI, tunaona Yesu alitumia tope kumponya kipofu, Paulo na Silah walitumia nyimbo na milango ya gereza ikafunguka, Musa alitumia fimbo kuwapitisha watu baharini, kwahiyo jambo hili la kutumia maji lilikuwa ni jambo la kiimani kwani tumeona Mungu akitenda miujiza kupitia vinywa vya watumishi wake.

Pia aliyaombea hayo maji na kuyageuza kuwa damu ya Yesu Kristo na aliwaomba watu wayanywe hayo maji na kuyanyunyizia katika mikono yao na miguu yao kwa imani.

Yawezekana unapitia changamoto mbalimbali na umehangaika huku na kule ukitafuta suluhisho la kutatua changamoto zako na hujabahatika kutatua, nataka nikwambie lipo jibu kwani Yesu mtenda miujiza yupo na anatenda kupitia watumishi wake. Sasa chukua hatua ya kufika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B ili ukutane na nguvu za Mungu, ujifunze Neno la Mungu, uombewe, na kama hujabatizwa ubatizwe. Ibada zetu katikati ya wiki ni saa 9 alasiri hadi saa 1 usiku na siiku ya Jumapili ni saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Biblia inasema katika kitabu cha Zaburi 84:4 Heri wakaao nyumbani mwako wanakuhimidi daima.


Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare




 Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

 Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare







 Kutoka kulia ni Mc. Daniel Kalege kutoka Uganda, Mch Elizabeth na Mch. Rosemary Mgetha
Mch. Stanley Nnko


















 Kutoka kushoto ni Bishop Dunstan Maboya, Mch. Noah Lukumay 

































Comments