RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

09.07.2017: WATU WALIOJIUNGA RASMI NA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

Bwana Yesu Asifiwe..
Naomba nikushirikishe ujumbe huu kutoka katika kitabu cha Nabii Isaya 1:18 inasema, "Haya, njooni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu, zitakuwa nyeupe kama theluji, zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi, bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga maana kinywa cha BWANA kimenena haya."

Tuna kila sababu ya kuwapongeza watu walioamua kujiunga na kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 09.07.2017, ikiwa ni siku ya hitimisho la semina ya siku 8 ya MID YEAR CROSS OVER. Watumishi hawa walikubali na kutii sauti ya mtumishi Mungu Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alipowaita watu wanaotaka kujiunga rasmi na kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ili waweze kujifunza Neno la Mungu na kupokea baraka za Mungu katika maisha yao. Tunamshukuru Mungu watu wengi waliweza kutii sauti ya mtumishi wake na kuamua kuchukua fomu za kujiunga na kanisa. Kwa kutii kwao tunaamini  wataanza kula mema ya nchi kama Biblia inavyosema katika Isaya 1:18.  Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuwaombea na kuwapa faida zinazopatikana kwa Yesu kupitia kanisa lake la Mlima wa Moto Mikocheni "B". 

Tunawapongeza sana watu hawa waliokubali kuja kanisani na kuweza kusemezana na Mungu kupitia vinywa vya watumishi wake. 

Tumeshuhudia watu wakipata mafanikio wakioa, wakipata safari za nje, wakipata kazi, wakiondolewa mapepo, wakifaulu masomo yao, wakipandishwa vyeo, wakipata promosheni, wakipata kibali katika mambo yao, wakilindwa na mengine kama hayo kwasababu wamemkubali Yesu kuwa BWANA NA MWOKOZI wa maisha yao.

Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare



 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare































Comments