MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

19.07.2017: DADA APOKEA UPONYA WA MAUMIVU YA MGONGO BAADA YA KUOMBEWA NA MCH. NOAH LUKUMAY

Mungu akisema, Anakuponya hakuna wa kukupinga kipokea uponyaji wako. Mungu akisema anafuta mateso yako basi hakuna atakayesema hapana. Mungu wetu ni mwema sana, anawapenda watu wote. Unachotakiwa kukifanya ni kuwa karibu Naye na kufuata maandiko yake, kuwapenda watu, kutotenda dhambi na kutenda yaliyo mema kila kuitwapo leo.

Siku ya Jumapili 19.07.2017 katika ibada ya KUPELEKA MASHITAKA YETU KWA MUNGU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", tulishuhudia Mungu akimponya dada aliyekuwa anasumbuliwa mgongo kwa muda mrefu. Hii ilitokea baada ya Mch. Noah Lukumay kuwaita watu wenye magonjwa mbalimbali waje katika madhabahu ya miujiza ya Yesu ili waombewe, na walipofika alimuita huyu dada ili amuombee. Wakati akimuombea, mapepo yalianza kumtoka huku akigalagala chini na kunyooosha mikono, akipiga kelele kutokana na nguvu za Mungu zilivyokuwa zikifanya kazi dhidi ya mwovu shetani.

Mch. Noah Lukumay na wachungaji wa kanisa hili waliendelea kukemea mpaka pale alipoweza kufunguliwa na kuwa huru, Baad ya kuombewa aliambiwa akatoe mkanda wake aliokuwa akiutumia kama "suport" kwake. Dada huyu alimshukuru Mungu kwa kumponya pamoja na wachungaji na kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" pamoja na waumini wote kwa maombi yao. Hivi sasa amepona kabisa na yuko huru.

Shetani amemtesa kwa muda mrefu sana, amehangaika bila ya kupata majibu, lakini alipokanyaga katika nyumba ya Mungu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" aliweza kupokea muujiza wake wa uponyaji.

Tunakuomba uendelee kufuatilia post zetu, kwani tutakupa historia ya ugonjwa wake alioupata akiwa ofisini kwake. Mungu akubariki sana.

Usisahau kuja kupokea muujiza wako Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha makumbusho aumMwenge kwenya mataa barabara ya Coca Cola Dar es Salaam.

Mch. Noah Lukumay (kulia)


0