MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

23.07.2017: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AKIOMBEA WATU KATIKA IBADA YA KUKOMESHA MAUMIVU SIKU YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Katika ibada ya KOKOMESHA MAUMIVU iliyofanyika siku ya Jumapili 23.07.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuwaombea watu wote waliofika siku hiyo. Ilikuwa ni Jumapili ya namna yake kwani kulikuwa na nguvu za Mungu. Watu walifunguliwa na kuondolewa maumivu katika mioyo yao. Tunamshukuru sana Mungu kwa kuokomesha maumivu katika mioyo ya watu iliyokuwa ikiumizwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na kukosa fedha, kuumizwa kimahusiano, magonjwa, kukosa mume/mke, matatizo katika ndoa, kukosa promosheni, kukosa kibali, umaskini, kuvamiwa na mapepo na majini, kusengenywa, kudhurumiwa, kuibiwa, kudaiwa, kutolipwa fedha zako, na mengine kama hayo. Mungu amekuwa mwema na tumeona akishughulika na maisha ya watu. Kupitia maombi yaliyofanyika katika hekalu hii watu kwa wiki hii wataanza kuona matokea chanya.

Ninachotaka kukutia moyo ni kwamba kwa Mungu hakuna lisilowezekana, ni wewe kufanya mapenzi yake, kuacha dhambi, kuwa na upendo, kutenda mema, kusoma Neno la Mungu na kulifanyia kazi, kusaidia wenye uhitaji, kuhudhuria ibada, kuwa mtoaji kanisani, kusamehe wabaya wako na mengine kama hayo.

Mwisho, ninaomba Jumapili hii usikose kushiriki ibada Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.


0