23.07.2017: HAPPY KWAYA MA JOYBRINGERS KWAYA ZA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" ZAGUSA MIOYO YA WATU KATIKA IBADA YA JUMAPILI

Happy Kwaya na Joybringers Kwaya zimefanyika baraka sana katika ibada ya KUKOMESHA MAUMIVU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 23.07.2017. Tulibarikiwa sana na ujumbe na jinsi walivyokuwa wanacheza kwaajili ya BWANA. Hakika tunaona uwepo wa Mungu tunapoona waimbaji hawa wakimtumikia Mungu kwa furaha. Siku ya Jumapili hii watakuwepo Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana wakimtukuza Mungu. Ungana na waimbaji hawa upokee upako kutoka kwao. Mungu akubariki sana.
0