MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

23.07.2017: MAMA ATOA SADAKA YA MALIMBUKO MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Mama aliyevalia gauni la rangi ya pink siku ya Jumapili 23.07.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwenye ibada ya KUKOMESHA MAUMIVU YETU aliweza kumshukuru Mungu kutokana na jinsi alivyomsaidia katika kilimo chake mpaka kufikia mavuno. Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la wachungaji waliweza kumshukuru Mungu na pia kumuombea mafanikio, ulinzi katika kilimo chake.

Kupitia huyu mama kuna kitu tunajifunza. Mungu anavyotubariki kwa kikubwa au kidogo tunapaswa kumshukuru ili azidi kutubariki. Pia unaposhuhudia mbele za watu tunasababisha na wengine kuzidi kumuamini Mungu kuwa ANAWEZA kumuinua mtu kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine. Tujenga tabia ya kushuhudia pale tunapoona Mungu ametutendea makuu katika maisha yetu. Shuhuda zinainua imani za watu na kuwaleta watu kwa YESU.

Mungu akubariki sana na nikukaribishe katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" saa asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye Mataa barabara ya Coca Cola....

 Kulia ni mama aliyemtolea Mungu sadaka ya malimbuko  na anayefuata ni Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
0