MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

23.07.2017: UJUMBE MZITO KUTOKA MLI A WA MOTO MIKOCHENI "B" - Mch. Noah Lukumay//Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata AKAMTOA Mwanae wa pekee, ili kila Mtu AMWAMINIYE asipotee bali awe na UZIMA wa milele// Yohana 3:16

KWAHIYO
>> Wewe usiyemwamini YESU, huna uzima wa milele

>> Wewe unayemwamini YESU una uzima wa milele

>> Wewe usiyeamini umepotea

CHAKUFANYA SASA

<< Chagua kupotea au kuwa na uzima wa milele>>

NAOMBA UJIBU SWALI HILI
>>Je, unamwamini YESU kama Unamwamini sema NDIYO na kama humwamini sema HAPANA ili tukusaidie<<

YESU ANAWEZA KUSEMA MANENO MACHACHE NA UKAPOKEA MUUJIZA WAKE..SOMA HII


Yohana 5:7-8: Yule mgonjwa akamjibu Yesu; "BWANA mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa, ila ninapokuja mimi mtu mwingine hushika mbele yangu. Yesu akamwambia, SIMAMA UJITWIKE GODORO LAKO UENDE. Mara yule mtu akwa mzima....

>> Yawezekana unaumwa, kila ukihitaji msaada hakuna wa kukusaidia, kila ukijitahidi ufikii kusudi lako juu ya ugonjwa wako. na pengine upo kitandani au kazini au njiani au kanisani au safarini au mitaani, au sebuleni, au chumbani au mahali popote pale ulipo unaumwa, unateseka, unalia, unawaza, unahisi kutengwa, unahisi kuonewa, umekata tamaa, umehangaika sana. Nataka nikwambie Yesu Kristo anasema Jitwike godoro lako na uende, wewe ni mzima.

Sasa naomba ufanye kitendo cha imani hapo ulipo..Mwambie Yesu, "Naomba uniponye sasa hivi" rudi tena na tena, halafu "Sema Asante Yesu kwa Kuniponya"

Simama ulipo na anza kufanya mzoezi ya kutembea kwa jina la YESU... Fanya vile ambavyo ulikuwa hufanyi kwa IMANI huku ukisema, "Asante Yesu kwa Kuniponya"

>>Mlima wa Moto Mikocheni "B" tupo mbali ila kupitia ujumbe huu UMEPONA. Muamini Yesu.....Endelea kusema asante Yesu huku ukifanya vile ambavyo ulikuwa hufanyi kwa jina la YESU KRISTO<<

Kwa uponyaji huo uliopata usikose kija nyumbani mwa BWANA Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana kuleta ushuhuda wako. Endelea Kumshukuru Mungu...


UKIPONA UGONJWA HUO UNAOKUSUMBUA, USITENDE DHAMBI TENA.

Yohana 5:14...Angalia umekuwa mzima, usitenda dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zadi..


Ninashangaa ninapoona mtu aliyepona katika ugonjwa uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu, anaendelea kutenda dhambi!!!. Watu wengi waliothubutu kutenda dhambi baada ya kuponywa na Yesu Kristo, wameishia pabaya sana. Unapomkose Yesu aliyekuponya ujue unamuudhi sana, anachukia sana, unamuumiza sana, unamuabisha sana, unamdharau sana, humtendei haki.

Yesu mwenyewe anasema kama wewe uliyeponywa ukitenda dhambi ujue mbele yako kuna jambo baya zaidi ya huo ugonjwa uliokuwa nao litakupata.....Kama wewe ulikuwa na UKIIMWI basi ujue utapata baya zaidi ya UKIMWI...Sasa sijui lilikupata utamuomba shetani akuponye au Yesu akuponye?

Niongee na wewe unayeumwa, unatakiwa kujua kuwa MPONYAJI ni Yesu tu, na kama ni YESU tu, basi usimsahau ukishapona. Anachotaka kwako wewe mgonjwa na wewe uliyeponywa ni kuacha dhambi maana ukitenda dhambi kuna baya zaidi ya huo ugonjwa utakumbana nalo..

Mungu akuponye wewe mgonjwa, na wewe uliyepona ugonjwa uzidi kutenda mema siku zote ili usikumbwe na baya kama utatenda dhambi. Mungu akusaidie usitende dhambi tena.

Nikukaribishe Mlima wa Moto Mikocheni "B" Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Ni siku yako ya kupokea uponyaji wako. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye Mataa barabara ya Coca Cola...

UNATAMANI KUTENDA KAZI ZA MUNGU LAKINI KILA UKIJITAHIDI HAKUNA ANAYEONA MCHANGO WAKO

Yohana 6:28: ...Tufanyeje ili tuweze kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu, akawaambia, "Hii ndiyo kazi ya Mungu, MWAMINI yeye aliyetumwa na yeye"


Kuna watu wanatamani kufanya kazi ya Mungu, lakini kila wakijitahidi kufanya hakuna mtu anayekubaliana na kile wanachokifanya. Inafika kipindi watu wanatumia njia zisizo za Mungu kufanya miujiza ili watu wawaamini kuwa wana nguvu za Mungu ndani yao kumbe ni mapepo yamo ndani yao. Mungu wetu ana taratibu zake ili akutumie kama chomo chake, na moja ya taribu hizo ni IMANI. Unaweza ukawa unatumia njia zako kulazimisha mambo yaende sawa lakini unaishia kutoa jasho tu, na hakuna chochote unachovuna. Muombe sana Mungu akusaidie kujua maana na IMANI au KUAMINI.

Leo hii Mungu anasema, UMWAMINI kwanza Yesu Kristo kwani yeye alitumwa kuja duniani kwaajili yetu. Kuna watu wengine hawajui KUAMINI ni kufanya nini? na ndio maana IMANI zao zimekuwa za mashaka sana. Inafika kipindi mtu anakuwa na imani za kipepo na hapo hapo anamtaja Yesu Kristo kama kivuli. Ndugu yangu nataka nikwambie hutafanikiwa katika huduma yako, hautaweza kutenda kazi za Mungu kamwe, na mwisho wake ni mbaya mbele za Mungu.

Njia fupi ya KUTENDA KAZI ZA MUNGU ni "KUMUAMINI TU" na kama hujui kuamini ni kufanyeje basi nakuomba Jumapili hii saa 3 asubuhi tukutane Mlima wa Moto Mikocheni "B" utaelewa maana ya "KUAMINI"0