MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

23.07.2017: WATU WALIOKOKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

Biblia inasema katika kitabu cha Mithali 29:25, "Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; bali amtumainiye BWANA atakuwa salama". Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuwapa ufunuo hawa ndugu zetu waliokoka siku ya Jumapili 23.07.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" baada ya kuona hakuna faida yoyote ya kuwategemea wanadamu na kuwaogopa kutoka na nguvu walizonazo kiuchumi au nguvu zozote zile walizonazo, wakaona ni vyema sasa kumtumainia BWANA wetu ili awe mlinzi wa maisha yao. Maamuzi ya kuokoka sio kitu kirahisi hasa kwa yule ambaye alikuwa hana mwanga wa wokovu, hii tunasema ni neema ya Mungu kuona mtu anachukua hatua za kuokoka. Unapoona umepata neema hii ya wokovu usiichezee kabisa kwani wapo watu wengi sana wanatamani KUOKOKA lakini wanashindwa kutokana na jinsi walivyobanwa na nguvu za giza, shetani amefunga macho yao hawaoni faida za kuokoka, hawaoni hatimaya yao baada ya kuondoka hapa duniani.

Ndugu zetu hawa waliamua kufika katika ibada ya KUKOMESHA MAUMIVU YETU iliyofanyika katika nyumba ya BWANA ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" na wakkamua kuokoka. Wachungaji waliwaongoza sala ya toba, waliwaombea, waliwabatiza kwa maji mengi na siku ya Jumatatu na Jumanne walianza masomo yao ya kukulia wokovu hapo hapo kanisani.

Wakati wakiombewa kanisani kabla ya kubatizwa, watu wengi sana walitokwa na mapepo, majini na nguvu za giza zilizokuwa zikiwatesa kwa kipindi kirefu. Na walipopelekwa kubatizwa kwa maji mengi wapo waliotokwa na mapepo na baadae kujazwa Roho Mtakatifu.

Niongee na wewe ambaye hujaokoka. Unayo nafasi sasa ya kuokoka, kesho sio kesho yako kwani ni kama giza. Hujui kitu gani kitakukumba baada ya hapo ulipo. Angalia maisha yako kama yako vizuri na Mungu, na fikiria Je, ukifa sasa una uhakika wa kwenda mbinguni? kama unaona huna uhakika, basi amua sasa kuokoka, na muombe Mungu siku ya Jumapili saa 3 asubuhi ufike Mlima wa Moto Mikocheni "B" watumishi wa Mungu wakuombee na kukuongoza sala ya toba na kukufundisha Neno la Mungu ambalo litakufanya ukomaa KIIMANI.

Mungu akubariki sana na tuonane Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye Mataa barabara ya Coca Cola...

Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye Mataa barabara ya Coca Cola...0