MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

23.07.2017: WATU WALIVYOBATIZWA SIKU YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Siku ya Jumapili 23.07.2017 katika ibada ya KUKOMESHA MAUMIVU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", watu wengi waliamua kuokoka na kumpokea Yesu kuwa BWANA na Mwokozi wa maisha yao. Wachungaji waliwaongoza sala ya toba, waliwaombea na baadae walibatizwa kwa maji mengi. Siku ya Jumatatu na Jumanne walianza masomo yao ya kukulia wokovu.

Ndugu zetu hawa wanahitaji sana maombi yako ili wasonge mbele katika wokovu. Maamuzi waliyofanya ni chukizo kwa shetani kwa hiyo wanahitaji sana ulinzi kutoka kwa Mungu. Maombi yako yatasababishwa shetani kushindwa kuwateka ndugu zetu hawa.

Pengine wewe ambaye hujaokoka ungetamani kuokoka, tunakukaribisha Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Watumishi wa Mungu watakuongoza sala ya toba, watakuombea, watakubatiza na kukufundisha Neno la Mungu..

Usafiri wa kufika kanisa ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola0